MKUU
wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga amepiga marufuku watumishi wa idara
ya Madini kwenda kusimamia na kukusanya mrabaha na kodi zote za
serikali katika mgodi wa Bulumbaka Gasuma na badala yake mgodi huo
utasimamiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama (KUU)
Kiswaga anadai watumishi hao wamepewa kazi hizo kinyemela na Kaimu Afisa wa Madini Mkoa wa Simiyu, Injinia Joseph Kumburu.
"Alikuwa naye mtu huyu Kahama (Shinyanga) huko katika Mgodi unaitwa Wime.
Amemleta
akusanye mapato hapa, eti ni kwa nini hiyo? Na huyo mtu ninayemsema
amepewa kazi kisheria kusimamia Dutwa Two. Pale haitoshi amemleta hapa
(Bulumbaka) kinyemela", alidai DC Kiswaga na kuongeza:
"Kwa
mujibu wa sheria alitakiwa kama anataka kumleta mtu yeyote hapa,
ashirikiane na maafisa wa kutoka Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye ni
Afisa Usalama wa Wilaya, Afisa wa Takukuru na Afisa OCD. Ndiyo
angeshauriana nao.
Lakini
hata kwa akili ya kawaida tu, hivi kweli Mhasibu atoke Kahama! Yaani
Simiyu yote hii haina....Bariadi yote hii haina mhasibu, Bulumbaka hii
hakuna mpaka atoke Kahama rafiki yake?"
Alisema
mgodi huo siyo mali ya familia, hivyo alimuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya
ya Bariadi (OCD) kuwakamata watu hao, punde watakapoonekana mgodini hapo
wakikusanya mapato ya Serikali.
Alisema wawili hao ni mafufuku kukanyaga mgodini hapo.
"OCD, OCD hao watu wakionekana hapa kamata weka ndani," alisema DC Kiswaga na kushangiliwa na wachimbaji hao wadogo.
Jitihada za kuwapata watu hao ili wazungumzie madai hayo ya DC Kiswaga, bado zinaendelea.
Katika
hatua nyingine, Mkuu huyo wa Wilaya ya Bariadi alitangaza hadharani
kuwa Mgodi huo wa Bulumbaka anautambua kuwa ni eneo la rush.
Akizungumza
suala hilo, Kaimu Afisa Madini Mkoa wa Simiyu, Joseph Kumbaru alisema
kwa Hana cha kuzungumza kwa sababu hakuwa na taarifa za Mkuu huyo wa
Wilaya kwenda katika mgodi huo.
"Kwa
Sasa siwezi kusema chochote kuhusu suala hilo, binafsi sina taarifa ya
huyo Mkuu wa Mkoa, hivyo naomba unipe muda tutazungumza wakati
Mwingine,"alisema Mhandisi Kumburu.
No comments :
Post a Comment