*Serikali kujenga miundombinu ya mawasiliano nchi nzima
Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv - Wanging'ombe
SERIKALI imesema kuwa wananchi kupata mawasiliano ni haki msingi
kutokana mawasiliano hayo yamekuwa njia ya uchumi katika karne ya 21 kwani uchumi huo unakuwa kiganjani kwa kutumia simu.Hayo ameseyama Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea wakati wa mikutano tofauti ya wananchi wa Jimbo la Wanging'ombe Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe alipofanya ziara ya kuangalia hali ya mawasiliano katika kata ya Ilembula,Imalinyi pamoja na Itambo.
Kundo amesema kuwa Jimbo hilo Wanging'ombe katika sehemu zenye changamoto za Mawasiliano mikakati imeshaanza kufanyika wa ajili ya kuweka minara.
Amesema Mbunge wa Jimbo hilo na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais-Tamisemi Dkt.Festo Dugange alimuomba afike katika maeneo yenye changamoto ya mawasiliano ambapo ameyaona na kuahidi kujenga miundombinu hiyo.
Aidha amesema serikali imedhamiria kuwa kila mwananchi anapata mawasiliano kwani ndio njia ya uchumi ambapo unatoka katika barabara na kuingia katika mawasiliano.
"Hatuna sababu itayofanya mawasiliano ya simu yasipatikane kwa wananchi huku tukitambua mawasiliano ndio uchumi wa sasa kwa serikali hii ya awamu ya Tano haiwezi kutokea kushindwa kufikisha mawasiliano"amesema Kundo.
Amesema Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuanzisha Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ni kutokana na maono ya mbali hivyo wasaidizi wake nikiwemo Naibu Waziri na Waziri lazima tuchape kazi ili dhamira ya Rais itumie kuanzisha Wizara hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Wanging'ombe na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais -Dkt. Festo Dungange amesema ujio wa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia Habari kwake ni neema ya kuweza wananchi wake wapate mawasiliano.
Dkt.Dugange amesema kuwa Jimbo hilo linafursa za kibiashara hivyo kufika kwa mawasiliano ni suluhu kubwa ya kufanya maendeleo hayo kwenda kwa kasi.
Baadhi ya wananchi katika mikutano ya Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo walimuomba kutatua changamoto ya mawasiliano kutimiza dhamira ya kufika katika jimbo hilo.
No comments :
Post a Comment