Monday, March 1, 2021

NAIBU WAZIRI MARY MASANJA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA KIUTALII MKOANI GEITA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (katikati) akiwasili kukagua hoteli ya Nyota 3 ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA) inayojengwa wilayani  Chato mkoani Geita wakati wa Ziara  yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya  mkoani Geita. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Eng. Charles Kabeho na kulia ni Kamishna Mwandamizi  wa Uhifadhi Kanda ya Magharibi, Martin Loibooki.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Robert  Gabriel kuhusu mpango wa Wizara ya Maliasili na Utalii wa kutaka kuanzisha Utalii wa Madini katika mkoa huo  wakati wa Ziara yake ya Kikazi  mkoani humo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kulia) akiwa anashuka kwenye hoteli ya Nyota 3 ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA) inayojengwa wilayani  Chato mkoani Geita wakati wa Ziara  yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya  mkoani Geita. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Eng. Charles Kabeho.

………………………………………………………………………………………………………

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja   amefanya Ziara katika mkoa wa

Geita ambapo pamoja na mambo mengine  amekagua miradi mbalimbali ya Kiutalii inayotekelezwa na Taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii  mkoani  humo. Akiwa katika ziara hiyo  amefanya mazungumzo na viongozi wa Serikali wa mkoa wa Mwanza na wale wa Taasisi zilizo chini ya Wizara  kuhusu  namna bora ya kutangaza Vivutio vya Utalii Vinavyopatikana katika mkoa huo.

Aidha, Mhe. Masanja ametembelea Mradi wa Ujenzi wa hoteli ya Kitalii ya Nyota 3 inayojengwa  wilayani Chato mkoani Geita na kuagiza ujenzi wa hoteli hiyo ukamilike haraka ili watalii waanze kupata fursa ya kutumia huduma za malazi katika hoteli hiyo na  kutembelea Hifadhi mbalimbali zilizopo kanda ya Ziwa.
Amesema Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kushirikiana na Uongozi wa Mkoa wa Geita kuhakikisha shughuli za  Utalii zinasonga mbele huku akitoa rai kwa Viongozi hao kuweka mkazo katika zao la asali ambalo amesema likisimamiwa Vizuri litaongeza mapato ” Tuhamasishe zao la asali linalotokana na Nyuki, sasa hivi kuna mnyororo mkubwa wa thamani ambao serikali inaendelea kuupigania kwenye mazao ya Misitu, hii itasaidia wananchi kuongeza kipato pia Pato la Taifa ” Amesema Mhe. Mary

Aidha,  ameongeza kuwa  Wizara ya Maliasili na Utalii  iko katika mpango wa kuanzisha Utalii wa Madini ambao kwa Kanda ya Ziwa utasaidia kuongeza idadi ya Watalii na Mapato.

 

No comments :

Post a Comment