Waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Dkt.Faustine Ndungulile akimkabidhi hati ya Ardhi Katibu mkuu wa Umoja wa Posts Afrika ,Katibu Mkuu wa umoja wa Posta Afrika (PAPU),Djibrine Younouss,kulia kwake ni Posta masta mkuu Hamisi Mwang'ombe.
Waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Dkt.Faustine Ndungulile akikagua hati ya kiwanja Cha PAPU Mara baada ya kukabidhiwa na kwa niaba ya Katibu mkuu
Kaimu Katibu mkuu wa Wizara ya Mawasiliano Injinia Clarence Ichekweleza akimkabidhi Waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Faustine Ndungulile hati ya kiwanja Cha PAPU leo Jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi Victor Nkya akitoa taarifa ya mradi wa makao makuu ya PAPU mbele ya Waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Dkt.Faustine Ndungulile
Na Vero Ignatus,Arusha
Hatimae
mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 25 baina ya (PAPU) na baadhi ya
wananchi wa kiwanja cha Makao makuu ya Posta Afrika kilichopo Mkoani
Arusha umetatulika baada ya kukabidhiwa hati rasmi kwa umiliki kwa PAPU
kuwa Mmiliki halali wa kiwanja hicho.
Akizungumza katika makabidhiano hayo ya hati Waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndungulile alisema hii Ni moja ya mafanikio makubwa ya kukabidhi hati na hatujawahi kutokea katika Jiji la Arusha na utaleta tija .
Amewataka
wakandarasi kuongeza kasi ya ujenzi huo kwnai wapo nyuma kwa wiki mbili
ambapo amesema anaimani kuwa ifikapo June mwakani jengo hilo litakuwa
limekamilika
"Niwasihi
wakandarasi mnaosimamia mradi huu muhakikishe unamalizika kwa wakati
kama ilivyopangwa mwezi wa sita ,2022 hivyo mhakikishe mnafanya kazi
usiku na mchana ili umalizike kwa muda uliopangwa na kw wakati sahihi "
amesema Dkt.Ndungulile
Amesema
kuwa, kukamilika kwa mradi huo kutaongeza ufanisi mkubwa katika
utendaji kazi wao huku ikitoa fursa mbalimbali za ajira pindi jengo hilo
litakapokamilika.
Amesema
kuwa ,mradi huo hadi kukamilika utagharimu kiasi cha shs 33.6 bilioni ,
ambapo aliipongeza wizara ya ardhi kwa kufanya kazi nzuri ya kukabithi
hati hiyo kwani kwa muda mrefu walikuwa hawana hati ya kiwanja hicho.
Dkt.Ndungukile
amelitaka Shirika la Posta kuwa kielelezo pekee cha maendeleo ambacho
kitakuwa mfano bora wa kuigwa huku akiwataka kwenda na kasi mpya ,na
kuhakikisha makao makuu ya posta yanafafana huduma wanazotoa katika
kuhakikisha inaendeshwa kidigitali zaidi.
Naye Mwenyekiti wa bodi kutoka TCRA,Dokta Jones Killimbe
amesema kuwa,ujenzi wa jengo hilo ambao ndio utakuwa makao makuu ya
posta Afrika na ofisi za Kanda ya kaskazini za PAPU ni ushindi mkubwa
Sana kwao kwani unaongeza ajira kwa watanzania walio wengi pia.
Dkt. Kilimbe amesema
kuwa,uwepo wa jengo hilo utaongeza tija kubwa kwa mapato ya fedha za
kigeni pamoja na kuwepo kwa mikutano yote ya Kimataifa ambapo ukumbi
utakuwa na uwezo wa kubeba zaidi ya watu Mia tano .
“Tunashukuru
sana kuongezewa eneo kwani lililokuwepo lilikuwa dogo Sana ila kwa Sasa
hivi eneo limepanuliwa na kuwa kubwa ,hivyo tunashukuru Sana kwa
serikali kwa ushirikiano mkubwa katika kukamilika swala hilo.”amesema.
Naye Katibu Mkuu wa umoja wa Posta Afrika (PAPU),Djibrine Younouss
amesema kuwa,anashukuru Sana serikali kwa kuwapatia hati hiyo baada ya
kuwepo kwa mgogoro kwa takribani miaka 25 Sasa na hivyo hivi Sasa
umeweza kufikia mwisho na kuweza kupatiwa hati hiyo.
No comments :
Post a Comment