Mkuu wa mkoa wa
Kilimanjaro Anna Mghwira akiangalia viatu wakati alipotembelea banda la
International Leather Industries Co. Ltd) lililopo Katika maonesho ya
nne ya programu ya uwezeshaji kiuchumi wananchi yanayofanyika Katika
viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.
Fredrick Njoka afisa
uhusiano wa ambaye pia ni meneja Masoko wa kiwanda cha bidhaa za ngozi
cha Kilimanjaro (Kilimanjaro International Leather Industries Co. Ltd)
akitoa maelekezo ya bidhaa ambazo wanatengeneza kwa wananchi
waliotembelea katika banda lao akiwemo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
………………………………………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Watanzania wametakiwa
kupenda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ikiwemo bidhaa za viatu
zinazozalishwa na kiwanda cha Kilimanjaro kwani vina ubora wa kimataifa
.
Hayo yamebainishwa na
Fredrick Njoka afisa uhusiano wa ambaye pia ni meneja Masoko wa
kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro (Kilimanjaro International
Leather Industries Co. Ltd) ambacho kinamilikiwa kwa ubia kati ya PSSSF
na Jeshi la Magereza kilichopo mkoani Kilimanjaro alipokuwa akiongea na
waandishi wa habari katika banda lao lililopo katika maonyesho ya nne ya
mifuko ya programu za uwezeshwaji wananchi kiuchumi yanayoendelea
mkoani Arusha.
Alisema watanzania
wanatakiwa kujua kuwa wanaposema Tanzania ya viwanda ni lazima waanze
kupenda na kuunga mkono vitu na bidhaa zinazotengenezwa na viwanda vya
hapa nyumbani,pia tuhamasishane watanzania wenyewe kwa wenyewe kupenda
vitu vya ndani.
Alisema kuwa kiwanda
hicho kimesaidia upatikana kwa soko la uhakika la ngozi ghafi kutoka kwa
wafugaji, Kuongezeka thamani ya ngozi inayozalishwa hapa nchini
kutokana na mpango wa mafunzo maalumu kwa wafugaji na ajira za moja kwa
moja 3000 na zaidi ya ajira 7000 zisizo za moja kwa moja katika mnyororo
wa thamani na huduma.
Alisema kiwanda hichi
kinasaidia Kuongeza mapato kwa Taifa kupitia kodi mbalimbali, pia kina
manufaa makubwa kwa mkoa wa Kilimanjaro pamoja na mikoa jirani kwa
kuboresha mfumo wa maisha na kuongeza kipato kwa wakazi, majengo na
miundombinu na kinaokoa fedha za kigeni kwa kupunguza uingizaji wa
bidhaa za ngozi nchini na kuongeza mapato ya fedha za kigeni kwa kuuza
bidhaa za ngozi nje ya nchi.
Alisema kuwanzishwa
kwa Kiwanda hiki cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro kumekuwa na manufaa
mengi kwa Taifa ikiwemo kuzalisha ajira nyingi kwa wananchi, kupunguza
matumizi ya fedha za kigeni pamoja na kuongeza wigo na thamani ya soko
la ngozi kwa wafugaji
Alibainisha kuwa
kiwanda hichi kinatengeneza soli za viatu jozi 2.1 na bidhaa mbalimbali
za ngozi kama vile Mikanda, Mabegi, Pochi, Mikoba na Majaketi ngozi
zenye ubora wa kimataifa na ubora wa uhakika ambapo alisema bidhaa zote
wanazitengeneza kwa bidhaa halisi ya ngozi za ng’ombe na mbuzi wa hapa
nchini.
“Watanzania waache
kuvaa bidhaa za mtumba plastic kwani bidhaa Kama za mtumba na za
plastic zinamathara makubwa Sana na zinaweza kuletea mtu mathara unaweza
unakuta unavaa kiatu Cha mtumba mtu alievaa huko kilipotoka labda
alikuwa na fangasi ukivaa na wewe unapata fangasi ,Sasa kuliko yote hayo
bora tujijengee tabia ya kuvaa viatu vipya vya ngozi ambapo tunabahati
maana tunakiwanda ambacho kinatengeneza viatu hivi hapa hapa
nchini”alibainisha Njoka.
No comments :
Post a Comment