Monday, February 1, 2021

WAIPONGEZA SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI UANZISHWAJI VIWANDA


Wafanyakazi kiwanda cha malti super brand wakiwa wanafanya kazi ya kupaki bidhaa tayari kupelekwa sokoni kama walivyokutwa na kamera ya matukio mjini Babati picha zote na Ahmed Mahmoud Manyara
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Malti Super Brand David mulokozi akiongea na vyombo vya habari kuhusu kiwanda kinavyozalisha
Moja wa taalam kiwanda hicho akipnyesha mitambo inavyofanya kazi kama wakati wanahabari walipotembelea kiwandani hapo mapema mwishoni mwa wiki picha zote na Ahmed Mahmoud Manyara
…………………………………………………………………………………………………
Na Ahmed Mahmoud Babati
Baadhi ya wafanyabiashara  Mkoani Manyara wameipongeza serikali kwa kuondoa urasimu katika uwekezaji wa viwanda ,Jambo lililowahamasisha kuanza ujenzi wa viwanda mbalimbali vya uzalishaji.
Mmoja ya wafanyabiashara hao ,David Mulokozi ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa kiwanda Cha kutengeneza vinywaji vikali Cha Mati Super Brands LTD kilichopo mjini Babati ,ameliambia gazeti hili kwamba Sera ya Rais John Magufuli ya Tanzania ya Viwanda imemfungua macho na kuamua kuanzisha Viwanda vya uzalishaji.
“Nilifanikiwa kufungua kiwanda kimoja Cha pombe kali Mwaka 2017 lakini hadi Sasa nifungua mefika viwanda vingine vitatu vya pombe Kali na pia nipo mbioni kufungua kiwanda kingine Cha dawa za binadamu baada ya serikali kuwatengenezea mazingira mazuri ya uwekezaji”amesema.
Amesema kuwa baada ya rais  Magufuli kuingia madarakani Mwaka 2015  na kuja na sera  ya ujenzi wa viwanda,Jambo hilo lilimhamasisha na kuamua kuanzisha kiwanda wilayani humo ambacho kimekua na kuzalisha viwanda vingine viwili na Sasa yupo mbioni kuanzisha kingine Cha dawa za binadamu
Amesema  viwanda hivyo vinazalisha vinywaji vikali aina ya Sed Pineapple Flavored Gin, Strong Dry Gin , Strong Coffee Flavored Gin New to be Launched na Tanzanite Premium Vodca.
Amesema kuwa tangu ameanzisha kiwanda hicho Mwaka 2017 amezalisha ajira zaidi ya 150 huku akitoa kipaumbele kwa wananchi wanaoishi jirani na kiwanda chake ikiwemo kuwajengea Mundo mbonu.
“Niliamua kuanzisha  kiwanda nikiwa na mtaji wa shilingi milioni 20 hasa baada ya kuvutiwa na sea ya Rais Magufuli  ya ujenzi wa viwanda ,Sasa hivi mtaji wangu umekuwa na wala sitegemei mkopo kutoka sekta za fedha “Alisema Mulokozi.
Amefafanua kwamba kabla ya kuanzisha kiwanda hicho alikuwa ameajiriwa kwenye kiwanda Cha mtu jijini Arusha kama afisa masoko lakini baada ya rais Magufuli kuanza kuhamasisha watu kujenga viwanda ,aliamua kuacha kazi na kufungua kiwanda chake mjini Babati.
“Tuimefungua vituo vya mauzo katika mikoa mbalimbali hapa nchini ikiwemo,Arusha, Kilimanjaro ,Tanga, Dar es Salaam, Morogoro,Mwanza na Mikoa mbalimbali hapa nchini na nchi jirani ya DRC Kongo,Kenya ,Rwanda,Zambia, Malawi, na Burundi”Amesema
Ameongeza kuwa matarajio yake ni kuwa na kiwanda kikubwa kinachoongoza kwa mauzo hapa nchini na ulipaji mzuri wa Kodi ya  serikali.
Amesema  Siri ya mafanikio ni usimamizi na ufuatiliaji pia kuajiri wataalamu wenye ujuzi ,kujua masoko na kuepuka kutegemea mikopo mikubwa katika kuendesha biashara yako.
Amewashauri wafanyabiashara wengine kutumia fursa hii ya raisi Magufuli kuanzisha viwanda na kutoogopa TRA kwani urasimu uliokuwapo hapo awali kwa Sasa umekwisha.

 

No comments :

Post a Comment