Monday, February 1, 2021

KALIUA WAANZA KULINDA KISHERIA ENEO LA KIHISTORIA LA MAKUMBUSHO YA MTEMI MILAMBO

Mkurugenzi Mtendaji wa Halamashauri wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua  Jerry Mwaga akijibu hoja mbalimbali za Madiwani jana .

Baadhi ya Majumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua wakiwa katika kikao cha kupitia hoja na taarifa za utekelezaji wa Kamati mbalimbali jana.
Picha na Tiganya Vincent

……………………………………………………………………………………………

NA TIGANYA VINCENT

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua imeanza mpango wa kuwekea mawe ya utambuzi wa eneo la mipaka ya makumbusho ya Mtemi Milambo kwa ajili ya kulilinda kisheria ili lisiweze

kuvamiwa na kupoteza histoaria yake.

Hatua hiyo inalengo la kuhakikisha kuwa eneo hilo lenye Historia kubwa hapa nchini linaendelea kuwa endelevu kwa ajili ya manufaa ya wakazi wa Kaliua na Taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halamashauri hiyo Jerry Mwaga wakati Baraza la Madiwani alipokuwa akijibu hoja ya Madiwani waliotaka maeneo yote ya vivuto vya Kihistoria na utalii kutunzwa kwa ajili ya kuongeza mapato ya ndani na Taifa  kwa ujumla

Alisema mbalimbali na eneo hilo wataendelea kuainisha maeneo yote ya kale na yenye vivutio kupitia vigezo vinavyotakiwa ili yaweze kutambuliwa na kulinda kisheria kwa lengo la kuwavutia watalii wa ndani na nje.

Diwani wa Kata ya Usimba Benjamin Masanja alishauri kuwa  maeneo ya kihistoria yaliyopo wilayani Kaliua yanatakiwa kuboreshwa na kuweka watu wanaoweza kuelezea kwa ufasaha historia ya eneo husika kwa ajili ya kuwavutia watu mbalimbali wanaofanya utafiti na wale watalii kuyatembelea.

Alisema  hatua hii itaiwezesha Halmashauri kupata mapato na baadhi ya wananchi kupata ajira ya kuongoza Watalii na watafiti watakaopenda kujifunza kuhusu utajiri wa historia ya mambo ya kale yaliyopo wilayani humo.

Naye Diwani wa Kata ya Kazaroho Haruna Kasele alishauri kuwa wakati umefika kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua ikaanza kuwekeza katika maeneo ya historia za kale ili kuvutia watalii wengi kutembelea maeneo husika.

Alisema hatua itawezesha Halmashauri hiyo kuongeza vyanzo vipya vya mapato ya ndani na kupata fedha kwa ajili ya kupeleka huduma za kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo utoaji wa huduma za afya , elimu na zile za ugani.

Kasele alisema Halmashauri ikiwekeza fedha kuboresha  Makumbusho ya Mtemi Milambo, eneo la kunyongea watumwa ambalo lilikuwa maarufu kwa jina la  Iselamagazi na njia ya Wajerumani  ambayo inaanzia Ndorobo wilayani Urambo kupitia Kazaroho wilayani Kaliua wataongeza mapato ya ndani.

 

No comments :

Post a Comment