******************************************
Taasisi ya Mifupa MOI kwa kushirikiana na Hospitali ya rufaa ya kanda ya kaskazini (KCMC) leo tarehe 05/02/2020 zimeanzisha ushirikiano wa kutoa huduma za kibingwa za upasuaji wa
ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu kwa wakazi wa kanda ya kaskazini ili kuwaondolea adha ya kusafiri umbali mrefu kuafuata huduma hizo Dar es Salaam au kwenda nje ya nchi.Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya rufaa ya Kanda KCMC Dkt Sarah Urasa amesema ushirikiano baina ya MOI na KCMC utaleta tija kubwa sio kwa wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro pekee bali kwa mikoa yote ya kanda ya kaskazini na nchi jirani ya Kenya ambao wamekuwa wakifika KCMC hapo kupata huduma.
“Kwanza niwashukuru ndugu zetu
kutoka MOI ambao wamefika hapa ili tushirikiane kuanzisha huduma hizi za
kibingwa za upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu,
tumekuwa tukitoa huduma hizi na sio kwa kiwango kikubwa hivyo kwa
kushirikiana na MOI tutakuwa tunatoa huduma hizi kwa kiwango kikubwa”
Alisema Dkt.
Sarah
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface amasema kuanzishwa kwa huduma za kibingwa za upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu katika hospitali ya KCMC ni azma ya Serikali ya awamu ya Tano ya kusogeza huduma za kibingwa kwa wananchi na kuwapunguzia adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma Dar es Salaam.
“Tumekuja hapa kwa ajili ya kuanzisha ushirikiano na wenzetu hawa wa KCMC katika eneo la upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu ili wagonjwa wenye magonjwa hayo wapate huduma hizo hapa pasipo ulazima kuja MOI, wataalamu wetu wamekuja kufanya tathmini ili tuwashauri namna bora ya kutoa huduma na pia kuwajengea uwezo wataalam wa hapa” Alisema Dkt. Boniface
Ushirikiano baina ya MOI na KCMC unatekeleza kwa vitendo azma ya Serikali ya awamu ya Tano ya kusokeza huduma za kibingwa kwa wananchi ili kuwapunguzia usumbufu wa kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo Dar es Salaam au nje ya nchi.
Tangu uhusiano huu wa tiba kati ya KCMC na MOI uanze tayari wagon jwa watatu wamepata huduma hii ya upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya hfahamu ambapo wangekwenda nje ya nchi serikali ya Tanzania ingelipa jumla ya milioni 135 wakati hapa KCMC matibabu yao yamegharimu jumla ya kiasi cha shilingi milioni 13
No comments :
Post a Comment