Wednesday, February 3, 2021

LINNA MARO JELA MIAKA 30 KWA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu mkazi wa Tabata, Lina Muro kwenda jela miaka 30 baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Agustina Mbando baada kupitia ushahidi wa

mashahidi saba wa upande wa mashitaka.

Inadaiwa kuwa Januari 26, 2018 huko Tabata Bima NSSF mshitakiwa huyo alikuwa akisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 43.95.

Katika hukumu hiyo Hakimu Mbando alisema, baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi wote Saba pamoja na vielelezo, Mahakama hiyo imejiridhisha pasipo shaka hivyo inamtia hatiani.

“Kwenye kesi za jinai mwenye jukumu la kuthibitisha pasipo shaka ni upande wa mashitaka baada ya ushahidi kutolewa,” alisema Hakimu Mbando.

Hakimu Mbando alisema kutokana na ushahidi wa Upande wa Mashitaka uliotolewa, Mahakama inamtia hatiani hivyo atatumikia kifungo cha miaka 30 jela pamoja na kutaifisha simu nne alizokutwa nazo.

Awali kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili wa utetezi Nehemia Nkoko aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa kuwa mtuhumiwa bado ni kijana na nguvu kazi ya Taifa na pia ana mtoto mdogo anaemtegemea.

Wakati huo huo, Hakimu Mbando amewahukumu watu wawili wakazi wa mbezi kwenda jela miaka 20 baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kuharibu miundombinu ya simu na kusababisha hasara ya Sh. Mil 25.

Wakazi hao ambao ni Rogers Festo (29) na Shafii Nampembe (43) wanadaiwa Septemba 16, 2018 maeneo ya Mbezi waliaharibu miundombinu ya simu ya TTCL kwa kukata nyaya na kusababisha hasara ya Sh. Mil 25.

“Baada ya kupitia kwa umakini ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa Jamhuri Mahakama hii imewatia hatiani kwa makosa mawili kufanya uharibifu wa miundombinu na kusababisha hasara,”alisema


 

 

No comments :

Post a Comment