*Ni Mashine ya Kisasa iliyopo katika Maabara ya TMDA Kanda ya Ziwa
Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Ziwa imesema mashine
ya LC,MS/MS. ina umuhimu katika uchunguzi wa sumu na kemikali katika Mwili wa Binadamu.Akizungumza na Waandishi wa Habari Katika Maabara ya TMDA Kanda ya Ziwa Kaimu Mkuu wa Maabara hiyo Bugusu Nyamweru, amesema mashine hiyo inafanya kazi na kuwa msaada katika ukanda huo.
Amesema katika mashine hiyo wanafanya uchunguzi mbalimbali pamoja na za utafiti za kawaida, chunguzi za kuangalia au kutambua kiwango cha kemikali na dawa ndani ya mwili wa binadamu.
Aidha amesema mashine hiyo Ina uwezo wa kufanya uchunguzi kwa kung'amua vitu vidogo sana katika Mwili wa Binadamu.
Hata hivyo amesema faida ya mashine hiyo wakati wa kufanya uchunguzi inauwezo wa kugundua vitu vidogo sana vilivyo katika mwili wa binadamu pamoja na kutambua kiasi cha kemikali katika sampuli yeyote.
Amesema kwa kawaida uchunguzi unafanyika mara mbili hadi pale kemikali imeweza kuchanganuliwa katika vipande ambapo mwisho kupata maumbile au kipande cha kinachotokana na bacteria wa aina fulani.
Nyamweru amesema kuwa mashine hiyo pia inaweza kutumika katika kupima uchafuzi katika dawa na mazingira ya dawa katika uhifadhi wake kwa kuangalia kiambata hai kwenye dawa.
Nyamweru amesema kuna kiambata kingine sio hai au kiambata hai kilichoharibika katika mwili.
“Tunafanya uchunguzi wa dawa inavyofanya kazi katika mwilini na hufanyika baada ya dawa kufika na mabaki yake kuangaliwa kwa umbo gani na yametengenezwa kwa kemikali ipi au kujua kwamba dawa iliyotumika katika mwili katika eneo fulani iko kwa kiasi gani katika mifumo ya mkojo au mate au katika tishu ya mwili na sehemu zingine kama kwenye Moyo,Ini iko kwa kiasi gani."amesema Nyamweru.
No comments :
Post a Comment