Nguruwe wa Mlengwa wa Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii(TASAF) kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini
Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora,Hoka Leta wakiwa katika banda lao.
Mlengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii(TASAF) kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini Wilaya ya Igunga
Mkoani Tabora,Hoka Leta akiwaonyesha jana waandishi wa habari banda la
nguruwe alizozipata kutoka na fedha za TASAF.
Mlengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii(TASAF) kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini Wilaya ya Igunga
Mkoani Tabora,Hoka Leta (kulia) akiwaonyesha jana Afisa Habari wa TASAF
Estomu Sanga (kushoto) banda la nguruwe alizozipata kutoka na fedha za
TASAF.
Mlengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF)
kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini Wilaya ya Igunga Mkoani
Tabora,Hoka Leta akiwaonyesha jana waandishi wa habari nyumba yake
aliyoijenga kutokana na miradi aliibua kutokana na fedha za TASAF.
Picha na Tiganya Vincent
……………………………………………………………………………..
NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA
FEDHA zinazotolewa na
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) zimemwezesha mlengwa wa mpango wa
kunusuru kaya masikini Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora,Hoka Leta
kuanzisha mradi wa ufugaji wa nguruwe wapatao 23 na kumwezesha kuw na
fedha za ukopeshaji wanachi wengine.
Mlengwa huyo alitoa ushuhuda huo
jana wakati viongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na
waandishi wa habari walipokuwa katika ziara ya kujifunga mafanikio ya
walengwa.
Hoka alisema baada ya kupata fedha za TASAF alianza kwa ununuzi watoto wa nguruwe mawili na ndipo walizaana na kufikia 23.
Alisema kupitia mradi
huo ameweza kujengwa nyumba ya kisasa na kukodi mashamba na kulima
mpunga ambapo amezalisha magunia 100 kwa kipindi cha mwaka jana.
Mlengwa huyo aliongeza
kuwa ufugaji wa nguruwe umemwezesha kupata kiasi cha shilingi
300,000/= hadi 500,000/= kulingana na soko wakati husika na kuongeza
kuwa wateja wake wakubwa wanatoa katika mikoa ya Arusha na Dar es
salaam.
Alisema pia kupitia
ufugaji wake amekuwa akikodisha madume ya ngurume kwa wafugaji wengine
wanaohitaji mbegu kwa gharama ya shilingi 15,000/= kwa mmoja ambapo
mradi huo nao umemsaidia kumudu maisha yake.
Aidha Leta alisema
kupitia kilimo hicho cha mpunga katika mavuno ya mwaka huu anatarajia
kuvuna zaidi ya gunia 100 za mpunga na mazao mengine.
Alisema kupitia fedha
za TASAF aliweza kuanzia kilimo cha zao la alizeti na kupata dumu 20 za
mafuta ya alizeti ambapo fedha alizopata zilimsaidia kununua vifaa vya
ujenzi ikiwemo saruji , mchanga , mbao na mabati.
Leta alisema kabla ya
kupata fedha za TASAF alikuwa akiishi maisha ya dhiki ambao alikuwa
akisubiri watu watupe ndala zilizochoka na ndipo yeye alizichukua kwa
ajili ya kuvaa.
Aliongeza kuwa dhiki
nyingine aliyokuwa akikabiliana nayo kabla ya kupata fedha za TASAF ni
pamoja na kutokuwa na uhakika wa chakula kwa kuwa alitegemea zaidi
biashara ya kutembeza viazi mitamu na ndipo alizalishe shilingi 500/=
kwa ajili ya familia yake.
Leta alisema kupitia
miradi yake iliyotokana na fedha za TASAF hivi anao uwezo wa kukopesha
watu mbalimbali fedha ambapo hadi hivi sasakuna watu anawadai zaidi
shilingi milioni 1.5.
Mlengwa huyo alisema ni vema kwa
walengwa wanaopata ruzuku kupitia mpango huo, kuzitumia katika
shughuli za uzalishaji mali kwa lengo la kujiua kiuchumi na kuachana
na umasikini na wasirudi nyuma .
Aliishukuru Serikali ya awamu ya
tano kwa kuwawezesha fedha za mpango huo na kufanikiwa kujitegemea na
kuilea familia yake ya watoto 7 .
Mlengwa huyo alisema
hata akitolewa katika Mpango huo hivi sasa hawezi kushindwa kujimudu
yeye na familia yake katika mahitaji mbalimbali.
No comments :
Post a Comment