Baadhi ya washiriki walioshiriki Kikao cha Waziri wa Madini Doto Biteko
na Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Bukreef kilichofanyika
katika ukumbi wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania
(GST).
Na Tito Mselem Dodoma,
Waziri
wa Madini Doto Biteko, ameitaka Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu
ya Bukreef ambayo inafanya kazi kwa ubia na Shirika la Madini la Taifa
(STAMICO) pamoja na kampuni ya Tanzam kukamilisha masharti waliyopewa na
Serikali ili wapatiwe leseni ya uchimbaji.

Hayo
yamebainishwa na Waziri Biteko leo Februari 02, 2021 alipofanya kikao
na wawakilishi wa kampuni hizo kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano
wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST).

Biteko amesema, Bukreef wanapaswa kulipa fidia kwa watu wote
wanaotakiwa kulipwa pamoja na kuwasilisha taarifa ya fedha ya kibenki
(Bank Statement) ili Wizara pamoja na Tume ya Madini ijiridhishe kama
kweli kiasi hicho cha fedha wanacho.

Imeelezwa
kuwa mkataba baina ya Bukreef na STAMICO haukuwa yenye usawa, kwa sasa
mikataba hiyo imerekebishwa ambapo STAMICO wameridhika na mkataba huo.

Aidha,
mkataba huo, unawapa kipaumbele STAMICO katika kazi ya uchorongaji
ambapo mkataba huo utakuwa na maslahi mapana kwa Taifa.

Pia,
Waziri Biteko amesema, Mabadiliko ya Sheria ya Madini yameleta chachu
ya maendeleo katika Sekta ya Madini ambapo amewataka Bukreef kulipa
fidia na kuwasilisha haraka mpango wa uzalishaji ili kazi zianze
kufanyika.

Kwa Upande
wake, Kaimu Mkurugenzi wa Tanzam, Khalaf Rashid amesema, kampuni ya
Bukreef ilikuwa inayumba lakini baada ya kuanza kushirikiana kwa pamoja,
tumeanza kuonesha mafanikio ambapo kampuni inaamini itazalisha kwa
faida.

“Nichukue fursa
hii kuwaomba viongozi wa Wizara ya Madini na Tume ya Madini, kwamba
mtupunguzie masharti mliyotupa kama kuanza uzalishaji ndani ya miezi
sita pia kumaliza zoezi la kuwalipa fidia wenye maeneo yao ndani ya
kipindi cha miezi sita,” alisema Rashid.

Rashid
aliongeza kuwa, Mgodi wa Bukreef umetenga zaidi ya Dola za Marekani
bilioni 25 kwa ajili ya kazi ya uchimbaji mara baada ya kuruhusiwa.

Kaimu, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba,
amesema, katika utoaji wa leseni, Sheria ya Madini inaonesha wazi kuwa
kila kwenye mita 1 ndani ya eneo la leseni unatakiwa uwe na kiasi cha
fedha kisicho pungua dola za Marekani 500.

Katika
hatua nyingine, kampuni ya Uchimbaji Madini ya Dhahabu ya MMC ya Mkoani
Morogoro, imeeleza kuwa mpaka sasa imewekeza zaidi ya bilioni 30 katika
eneo ambalo walitengewa wachimbaji wadogo ambapo wanauhakika wa
kuzalisha kilo 30 za dhahabu kwa mwezi endapo watapatiwa leseni ya
uchimbaji katika eneo hilo.

uongozi wa kampuni hiyo umemueleza Waziri wa Madini kuwa, mpaka sasa
kampuni hiyo imetoa zaidi ya ajira 300, imechangia ujenzi wa barabara na
imetoa ahadi ya kujenga kituo cha Afya pamoja na Shule katika eneo
linalozunguka mgodi huo.

Naye,
Naibu Waziri wa Madini, Prof. Shukrani Manya amewataka wawekezaji
kufuata kanuni, taratibu na sheria zilizowekwa na Serikali wakati
wanapohitaji leseni ili kuondoa migogoro isiyokuwa ya lazima.

Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila, maeneo yote
yaliyotengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo lazima wachimbe wachimbaji
wadogo vinginevyo inatakiwa kampuni husika ielewane na wachimbaji
waliokuwepo ili wachimbe kwa kushirikiana na Wizara ijiridhishe ndiyo
Tume itaweza kutoa leseni kwenye maeneo hayo.

No comments :
Post a Comment