Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe akiongea na menejimenti na watumishi wa EPZA alipofanya ziara akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa Wizara ya Viwanda na Biashara
Mkurugenzi Mkuu wa EPZA Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia akipokea maelekezo kutoka kwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe (hayupo pichani) alipotembelea na kuongea na menejimenti na watumishi wa Mamlaka hiyo hivi karibuni akiambatana na Naibu Waziri wa Viwanda Mhe. Exaud Kigahe pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa Wizara ya Viwanda na Biashara
……………………………………………………………………………………
Dar es salaam
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe (Mb) ameiagiza Mamlaka ya Maeneo
Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) kujikita katika ujenzi wa maeneo mapya ya viwanda kulingana na biashara iliyopo katika mkoa husika ikianza na Mikoa ya Lindi, Mtwara na Pwani kwa ajili ya kuwawezesha wajasiliamali wadodo kuchakata korosho ikifuatiwa na maeneo mengine yayozalisha pamba kwa wingi pamoja na uchenjuaji madini
Waziri Mwambe aliyasema hayo alipokuwa akiongea na menejimenti na wafanyakazi wa EPZA alipofanya ziara katika taasisi hiyo akiambatana na Naibu Waziri wa Viwanda Mhe. Exaud Kigahe (Mb) pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa Wizara ya Viwanda na Biashara.
Aidha Waziri Mwambe pia ameiagiza EPZA kuyaendeleza na kuyatunza maeneo yote inayoyamiliki ambayo imeshayalipia kwa ajili ya ujenzi wa viwanda pamoja na kufuatilia madeni yote inayowadai wapangaji wake ili fedha hiyo itumike katika kuendeleza maeneo ya viwanda na kufikia malengo iliyojiwekea ambayo hayajafikiwa hadi sasa.
Vilevile Mhe. Waziri aliwaasa watumishi wa EPZA kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kuepuka vitendo vya rushwa wanapowahudumia wafanyabiashara pamoja na kujieendeleza katika taauma zao ili kuendana na wakati, kuweza kutoa huduma bora katika uwigo mpana wa biashara na kuongeza idadi ya wafanyabiashara wanaowahudumia.
Naye Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara aliisisitiza EPZA kuyaendeleza maeneo inayoyamiliki ili kuepusha migogoro ya ardhi na wananchi wanaovamia maeneo hayo pamoja na kutunza maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda kwa kizazi kijacho.
Aidha, Naibu Waziri aliiasa EPZA kushirikiana na TAMISEMI katika kuelimisha wananchi faida za maeneo ya EPZA yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda huku akiishauri kutumia fursa zinazojitokeza katika kuendeleza miundombinu katika maeneo hayo hususani barabara, maji na umeme.
No comments :
Post a Comment