WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa akiwa kwenye kiwanda cha Ihemi kilichopo mkoani Iringa kinachomilikiwa na chama cha mapinduzi akiangalia namna mafundi wanavyoshona nguo mbalimbali
Mkurugenzi wa kampuni ya Asas na mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (MNEC) Salim Abri Asas akiwa kwenye moja ya mikutano ya ndani ya chama cha mapinduzi
……………………………………………………………………………..
Na Fredy mgunda,Iringa.
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa amempongeza mkururugenzi wa kampuni
ya Asas Salim Abri Asas kwa jitihada zake za kuleta maendeleo mkoani
Iringa kwenye sekta mbalimbali.
Akiwa kwenye ziara ya
kukagua mradi wa chuo cha Ihemi na kiwanda cha Ihemi vinavyomikiwa na
chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa, mheshimiwa waziri mkuu alisema kuwa
kila akienda kukagua miradi ya maendeleo mkoani Iringa lazima akutane na
mchango wa Salim Abri Asas katika mradi huo.
Alisema kuwa
mkurugenzi huyo wa kampuni ya Asas na mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa
ya chama cha mapinduzi (MNEC) amekuwa akitolea kusaidia kukuza
maendeleo ya mkoa wa Iringa kwa ujumla.
Mheshimiwa
waziri mkuu alisema kuwa mchango wa MNEC Salim Abri Asas katika chuo
cha Ihemi ni mkubwa sana unapaswa kuheshimiwa kweli kweli maana
kujitolea kujenga majengo ya chuo na kiwanda sio jambo ambalo linapaswa
kupuuzwa kabasi hapa nchini.
Alisema kuwa kwa
naiba ya serikali anachukua fursa na kumshukuru na kumpongeza MNEC Salim
Abri Asas kwa uchango wake ambao unaongeza ajira n kukuza maendeleo kwa
wananchi wa mkoa wa Iringa kwa ujumla.
“Kila wakati nikija
kwenye ziara mkoani Iringa lazima nikutane na jina la Salim Abri Asas
kwenye shughuli za kimaendeleo tena akiwa ametoka mchango unaozidi
asilimia zaidi ya themanini hivyo mtu kama huyu anapaswa kuheshimiwa kwa
mchango wake “alisema
Akiwa katika kiwanda
cha Ihemi waziri mkuu aliutaka uongozi wa kiwanda hicho kuimalisha
ulinzi ili kuzitunza Mali zote za kiwanda kutoibiwa tena kama ilivyokuwa
hapo awali.
Awali akisoma risala
kwa mgeni rasmi katibu mkuu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi
taifa,MWL Raymond Mangwala alishukuru mchango mkubwa uliotewa na MNEC
Salim Abri Asas katika haraka za kufanikisha kukifufua chuo na kiwanda
cha Ihemi kwani bila mchango wake basi chuo na kiwanda visingekuwa
hivyo.
Alisema kuwa kwa
asilimia kubwa mashine zinazotumiwa kwenye Kiwanda hicho zimenunuliwa na
MNEC Salim Abri Asas na amejenga majengo mengi hapo ukianzia ukumbi
madarasa na jengo la kuwa kwa asilimia kubwa ni mchango wa MNEC huyo.
Mangwala
alisema kuwa wanachama wa chama cha mapinduzi na wananchi wote
wanapaswa kuheshimu na kuthamini mchango wa MNEC Salim Abri Asas kwenye
maendeleo ya uchumi katika mkoa wa Iringa.
Nao
baadhi ya vijana wa ccm mkoa wa Iringa walimpongeza MNEC Salim Abri
Asas kwa kazi kubwa anayoifanya mara kwa mara kuhakikisha chama cha
mapinduzi kinaimarika kila siku na kinaongeza wanachama wapya kila
uchwao.
Walisema
mkoani Iringa kila sekta MNEC Salim Abri Asas amechangia shughuli za
kimaendeleo kama vile sekta ya
michezo,miundombinu,afya,kilimo,elimu,uwekezaji,mawasiliano,viwanda na
kadharika hivyo wananchi wanapaswa kumpa heshima yake.
No comments :
Post a Comment