Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akijibu hoja za Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Taasisi za Wizara yake baada ya Kamati hiyo kupokea Muundo na Majukumu ya Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo Januari 26, 2021 Jijini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Abdallah Ulega na Kushoto ni Katibu Mkuu na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Abdallah Ulega akitoa maelezo kuhusu hoja mbalimbali zilizohojiwa na Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Taasisi za Wizara yake baada ya Kamati hiyo kupokea Muundo na Majukumu ya Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo Januari 26, 2021 Jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Innocent Bashungwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Stanslaus Nyongo ambaye ni Mbunge wa Maswa Mashariki akizungumza baada ya kupokea taarifa ya Taasisi za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo zilizowasilishwa na Wakuu wa Taasisi hizo kwa kamati hiyo Januari 26, 2021 Jijini Dodoma .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifafanua masuala mbalimbali yaliyowalisilishwa na wajumbe wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Muundo na Majukumu ya Taasisi za Wizara hiyo Januari 26, 2021 Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakiwa katika kikao cha kupokea Muundo na Majukumu ya Taasisi za Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo hiyo Januari 26, 2021 Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara yake baada ya kumaliza kikao na Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Muundo na Majukumu ya Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo Januari 26, 2021 Jijini Dodoma.
…………………………………………………………………………..
Na Shamimu Nyaki – WHUSM,Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amesema ubuninifu
wa kitendaji unaofanywa katika Taasisi za Wizara hiyo unaendelea kuleta mafanikio kwa wadau na Taifa.
Mhe.Bashungwa ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati ilipopokea taarifa ya Muundo na Majukumu ya Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo.
Akiendelea kuzungumza, Mhe. Waziri Bashungwa amesema kuwa lugha ya Kiswahili inaendela kukua na imeendelea kutangaza nchi yetu.
“Ushirikiano kati ya COSOTA na TCRA ni jambo la msingi katika kusimamia kazi na maslahi ya wasanii ikiwemo kupatikana kwa mapato yanayotokana na kazi zao” alisema Mhe. Bashungwa.
Kwa upande Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Abdallah Ulega ameishukuru Kamati hiyo kwa mawazo na michango yao katika kusimamia Sekta zilizochini ya wizara hiyo pamoja na Taasisi zake, huku akiwashauri wajumbe hao kuwa mstari wa mbele katika kukuza michezo katika maeneo wanayotoka pamoja na kusimamia maadili mila pamoja na desturi za nchi.
“Kesho Taifa Stars itakua uwanjani dhidi ya timu ya Guinea katika muendelezo wa mashindano ya CHAN, nawasihi Watanzania tuiombee na kuitia moyo timu yetu na tusiwe watu wa kuishambulia kwakua ni vijana ambao tumewaamini katika kuiwakilisha nchi yetu” alisema Mhe.Ulega.
Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Stanslaus Nyongo ambaye ni Mbunge wa Jumbo la Maswa Mashariki amelipongeza Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kutoa habari zenye ukweli na uhakika kwa wananchi, huku akilipongeza Baraza la Kiswahili la Taifa ( BAKITA) kwa kuendelea na kukuza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi.
Katika kikao hicho Wajumbe wa Kamati hiyo wametoa maoni ya kuendeleza Sekta na Taasisi za Wizara hiyo ikiwemo kuongeza ubunifu, rasimali watu na miondombinu ya kufanyia kazi pamoja na kusimamia vyema maslahi ya wadau inayowasimamia katika kuongeza vipato vyao pamoja na kukusanya mapato ya Serikali.
No comments :
Post a Comment