………………………………………………………………………………………
Na Zuena Msuya, Pwani
Watumishi wa Wizara
ya Nishati, wamesema kuwa wamefurahia sana ziara ya kutembelea Mradi
wa kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere(JNHPP) Mkoani Pwani.
Ziara hiyo ya Siku
tatu imeratibiwa na Uongozi wa Wizara ikisimamiwa na msimamizi wa Mradi
huo kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Christopher Bitesigirwe kwa
kushirikisha watumishi kutoka Idara na vitengo mbalimbali vya wizara
hiyo.
Wamesema kuwa ziara
hiyo imekuja wakati muafaka na imekuwa na ufanisi mkubwa kwa kuwa
wamejifunza na kujionea hali halisi ya kinachoendelea katika mradi huo.
Watumishi hao
wamesema kuwa wanaushukuru sana Uongozi mzima wa Wizara kwa kuridhia na
kuwawezesha watumishi wake kutembelea mradi huo pamoja na yule aliyetoa
wazo la watumishi kutembelea mradi huo na waliounga mkono.
” Sisi watumishi
tunajisikia fahari na kujivunia sana kwa kuwa sehemu ya mradi huu kwa
kuuona kwa macho yetu na vitendo, utekelezaji wake tangu hatua za awali
na si kwa maandishi wala kusimuliwa,
Hakika tutapata cha kueleza vizazi vyetu hapo baadaye “, Walisema Watumishi hao.
Watumishi hao
walienda mbali zaidi kwa kusema kuwa, huo ni mwanzo mzuri kwa Wizara
yao, na wanaimani itaendelea kuwashirikisha kwa kuwapa ridhaa ya
kutembelea katika miradi mingine inayoendelea kutekelezwa.
Hata hivyo walieleza
kuwa utaratibu huo umeongeza chachu ya kuitendaji kwa watumishi hao
kufanya kazi kwa kasi kubwa, Ubunifu, Umakini zaidi na kwa usahihi na
kujiona ni sehemu ya Mradi huo.
Ziara hiyo ya Siku
tatu inahusisha Watumishi wote wa Wizara ya Nishati kutoka Idara na
Vitengo mbalimbali ambao hutembelea mradi huo kwa awamu tofauti na
katika Makundi.
No comments :
Post a Comment