…………………………………………………………………………………
Na MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
KITUO cha afya
MEDWELL kilichoko halmashauri ya mji Kibaha ,mkoani Pwani kimetoa huduma
bure za upasuaji wa mtoto wa jicho kwa zaidi ya wagonjwa elfu mbili
,katika kipindi cha mwaka jana na mwaka huu mwezi januari 2021.
Pamoja na upasuaji
huo wa mtoto wa JIcho , pia kituo hicho kimeendesha zoezi maalumu la
kutoa matibabu bure na upimaji wa magonjwa ya akina mama ikiwa ni
pamoja na upimaji wa saratani ya mlango wa shingo ya kizazi.
Mkurugenzi mkuu wa
kituo hicho Bashiru Khaki, anasema kambi hiyo ni ya siku mbili ambapo
walilenga kuhudumia wakina mama na jamii.
“Wingi wa wakinamama
waliojitokeza kupata vipimo na matibabu baada ya kutangaziwa kuna huduma
hii ya bila malipo limeonyesha picha kuwa kuna uhitaji mkubwa wa
huduma za afya, hivyo tunajipanga kutoa huduma hizi mara kwa mara ili
wananchi wawe na afya njema na waweze kufanya kazi na kuinua uchumi wa
nchi, alisema, Khaki
Kwa upande wa huduma
ya macho pamoja na upasuaji wa mtoto wa Jicho, mkurugenzi huyo alisema
huduma hiyo hutolewa kila siku ya jumanne na ijumaa na kuwa siku zote
hutolewa bure.
Amina Ramadhani ni
meneja rasilimali watu, anasema zoezi hilo lilipangwa kufanyika kwa muda
wa siku moja lakini kutokana na wingi wa wagonjwa litafanyika Siku
mbili , jumamos na jumapili.
” Medwel tumejikita
zaidi kuhudumia jamii hususani katika suala zima la afya, hapa tunatoa
huduma za vipimo mbalimbali ,xray na ultrasound, pia upasuaji , huduma
za kulaza wagonjwa na nyingine nyingi, pia tunachimba visima na hata
katika suala la elimu pia tunachangia, lengo ni kuisaidia serikali yetu
katika kuimarisha afya ya wananchi wake,” alisema Amina
Mganga mkuu wa mkoa
wa Pwani Dr. Gunini Kamba ,alipongeza kituo hicho kwa jinsi kinavyounga
mkono juhudi za serikali katika suala la afya kwa wananchi wake na kuwa
serikali itaendelea kushirikiana nao pia akavitaka wadau wengine wa
afya wajitokeze kufanya huduma kama hizo.
No comments :
Post a Comment