Kaimu
Msajili wa Bodi ya Maziwa Ndugu, Noely Byamungu ( kulia) akiwa kwenye
kikao na mwekezaji wa Shamba la Ng'ombe wa Maziwa la Shafa Ndugu,
Mohammed Al-Alhazi (kushoto) na timu ya wataalamu wa Bodi ya Maziwa
(hawapo pichani) tarehe (6.1.2021) kwa lengo la kuangalia uzalishaji wa
maziwa unaofanywa na Mwekezaji huyo mkoani Iringa.
Kaimu
Msajili wa Bodi ya Maziwa Ndugu, Noely Byamungu ( wa kwanza kushoto)
akipata maelezo ya utunzaji wa ng'ombe kutoka kwa Ndugu, Mohammed Al-
Alhazi ( katikati) wakati alipotembelea shamba hilo lenye ng'ombe
takribani 400 wanaozalisha maziwa Lita 7500 kwa siku. Wa kwanza kulia ni
Afisa Usindikaji Bodi ya Maziwa, Bi. Fathiya Rashid.
Baadhi ya Ng'ombe wakiwa katika maeneo yanapofugwa.
KAIMU
Msajili wa Bodi ya Maziwa Ndugu, Noely Byamungu ametoa rai kwa
wawekezaji nchini kuwekeza kwenye ufugaji wa Ngo'mbe bora Maziwa ili
kuongeza uzalishaji wa maziwa nchini.
Hayo amesema jana (6.1.2021) wakati alipomtembelea mwekezaji wa shamba la Ng'ombe wa Maziwa la Shafa lililopo jijini Iringa.
Ndugu
Byamungu amesema kuna fursa kubwa katika ufugaji wa ngo'mbe wa maziwa
na hivyo wawekezaji hawana budi kuwekeza kwenye ufugaji wa ng'ombe bora
wa kisasa wanaozalisha maziwa mengi.
Ndugu
Byamungu alisema hadi sasa uzalishaji wa maziwa nchini umefika lita
bilioni 3.0 tu kutokana na ufugaji wa ng'ombe wa asili.
Kati
ya lita hizo, lita bilioni 2.1zinatokana .net ngo'mbe wa asili na lita
bilioni 0.9 za maziwa zinatokana na ngo'mbe wa kisasa.
Natoa wito kwa wadau wa sekta ya maziwa kuwekeza kwenye ufugaji wa Ng'ombe wa kisasa ili kuongeza uzalishaji" Alisema Byamungu
Sambamba
na hilo Byamungu alimpongeza mwekezaji huyo kwa jitihada kubwa
alizofanya za kuinua Tasnia ya Maziwa nchini kupitia ufugaji wa ng'ombe
bora wa kisasa wa maziwa.
Nae
Mwekezaji wa Shamba la Shafa Ndugu, Mohammed Al -Alhazi ameishukuru
Bodi ya Maziwa kwa kutembelea shamba lake na kwamba huu utakuwa mwanzo
mzuri wa Bodi kujenga mahusiano mazuri na wadau.
" Sisi kama wawekezaji tunashukuru sana bodi ya maziwa kwa ushirikiano huu mnaoendelea kutupatia" Alisema
Amesema
changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni usalama wa mifugo kwani
wananchi hupita kwenye eneo la Shamba hali inayoweza kusababisha
magonjwa ya mlipuko na hivyo kuhatarisha afya ya mifugo.
Aidha
, Mwekezaji huyo amesema lengo la shamba ni kuwa na Shamba bora la
ngo'mbe wa maziwa Afrika Mashariki kwa kuongeza idadi ya ng'ombe wa
maziwa kutoka 400 waliopo hivi sasa hadi 1000 ifikapo mwisho wa mwaka
huu.
Shamba la Shafa lilianzishwa mwaka 2019 likiwa na takribani ya ngo'mbe wa maziwa 120 tu.
Hadi
sasa shamba hilo lenye ekari 2500 lina ndama 142 na ng'ombe wa maziwa
wapatao 400 wanaotoa wastani wa Lita 27 za maziwa kwa ng'ombe na hivyo
kufanya jumla ya Lita 7500 za maziwa kukamuliwa kwa siku.
No comments :
Post a Comment