Thursday, January 7, 2021

TCRA YAWANOA POLISI MKOA WA KIPOLISI RUFIJI


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Rufiji Onesmo Lyanga akizungumza na Askari wa Mkoa wa Polisi huo wakati akifungua mafunzo ya kufanya tathimini na ufatiliaji wa makosa ya kimtandao yaliyofanyika wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Rufiji Onesmo Lyanga (katikati) akijadiliana Jambo Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero (kushoto) na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Kimtandao Joshua Mwangasa Mara baada ya kufungulia mafunzo kwa Askari wa Mkoa wa Kipolisi Rufiji.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akizungumza kuhusiana na mafunzo ya kufanya tathimini na ufatiliaji wa Makosa ya Kimtandao kwa Askari wa Mkoa wa Kipolisi Rufiji yaliyofanyika wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Askari Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wakiwa katika mafunzo ya kufanya Tathimini na Ufatiliaji wa Makosa ya Kimtandao yaliyofanyika wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Kimtandao Joshua Mwangasa akitoa mada kuhusiana na Makosa ya Kimtandao
Mhandisi Mwandamizi wa Christopher  John akitoa mada katika mafunzo ya Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji.
Mwanasheria Mwandamizi wa TCRA Vaolet Eseko akitoa mada kuhusiana na sharia za mawasiliano kwa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Rufiji.

Kamanda Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Rufiji Onesmo Lyanga akiwa katika picha za pamoja za makundi ya Askari Polisi wa Mkoa huo Pamoja watendaji wa TCRA Mara baada ya kufungu mafunzo.

*Kamanda Lyanga asema watakwenda kisasa  kukabiliana na  wahalifu wa

Makosa ya Kimtandao

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Mkuranga 

JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji limesema kuwa wahalifu wa Makosa ya  Kimtandao wa mbinu nyingi lakini Polisi watakwenda kwa mbinu zingine za kisasa.

Hayo aliyasema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji Onesno Lyanga  wakati akifungua mafunzo ya Tathimini na ufuatiliaji wa Makosa ya Kimtandao kwa askari Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Rufiji yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki.

Kanda kwa askari wa Makosa ya Kimtandao  iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki  yaliyofanyika wilayani  Mkuranga mkoani Pwani.

Kamanda Lyanga  amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwani wahalifu wanambinu nyingi hivyo kukutana na TCRA kunajenga uimara na kufanya kazi hiyo kwa weledi kwa Polisi na kuhudumia wananchi na kutoa elimu kwa kutumia mawasiliano salama.

Lyanga  amesema kuwa pale wanapokuwa wamepata taarifa za mwananchi dhidi ya kufanyiwa uhalifu wa kimtandao huo wanachukua hatua za haraka ikiwemo kuwasiliana na watoa huduma za mawasiliano.

 Amesema mifumo ya ufatiliaji wa makosa na sheria zimeboreshwa ikiwa ni kumlinda mwananchi katika kupata huduma salama na sio kufanyiwa uhalifu na matapeli.

"Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji  tutaendelea kushirikiana  na TCRA katika utoaji wa huduma kwa wananchi kwa ubora kwa kuhakikisha wananchi wanahudumiwa kwa  weledi pale taarifa za kufanyiwa utapeli wa Makosa ya Kimtandao zinapopatikana na hiyo ni  pamoja  na kuwafikisha katika vyombo vya sheria"amesema Lyanga.

Naye Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi  Lawi Odiero amesema kuwa utoaji elimu ni endelevu kwani kadri ya Teknolojia inavyobadilika ndivyo wahalifu wanabuni mbinu zingine ikiwa ni Pamoja na wananchi kuendelea kupata elimu ya mawasiliano.

Amesema kuwa TCRA imejipanga katika kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali katika kwenda sambamba na ukuaji wa Teknolojia ya Mawasiliano kwa Kasi kwa kuweka mifumo ya kuweza kukabiliana na wahalifu.

Mhandisi Odiero amesema wananchi wanatakiwa wanapofika Polisi wanapata huduma kutokana na Polisi kuwa na mafunzo mbalimbali ya kuhusiana na mawasiliano na Pamoja na Makosa ya kimtandao.

Kwa Upande wa Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Mtandao wa Jeshi la Polisi Makao Makuu Joshua Mwangasa amesema kuwa kutokana na elimu Makosa yanapungua kutokana na kuwepo kwa elimu kwa Askari wa Jeshi la Polisi katika kukabiliana na wahalifu wa Makosa ya Kimtandao.

Amesema uchunguzi wa Makosa ya kimtandao una mambo mengi wakati mwingine yanavuka mipaka ya nchi kupata taarifa.

Amesema kuwa mafunzo waliyoyapata askari watatoa huduma bora kwa wananchi wanapokwenda kutoa taarifa za  Makosa ya kimtandao.

 

No comments :

Post a Comment