Na Woinde Shizza,Arusha
WANANCHI
Sita wameuawa na wengine saba kujeruhiwa vibaya kwa kushambuliwa na
Tembo katika Kijiji Cha Makuyuni wilaya ya Monduli ,Mkoani Arusha katika
kipindi cha miaka miwili na kusababisha wakazi wa Kijiji hicho kuishi
kwa hofu.
Aidha
Tembo hao wanadaiwa kuvamia pia mashamba ya wananchi hao na kufanya
uharibifu wa mazao yao jambo lililosababisha wakose chakula katika
kipindi Cha miaka miwili na kuishi maisha ya tabu.
Hayo
yameelezwa jana na Mwenyekiti wa Kijiji Cha Makuyuni,wilayani humo
Ngayoo Measi katika mazishi ya Mkazi mmoja wa Kijiji hicho, Ester
Sindiyo (55) aliyeuawa na Tembo Desemba 21 mwaka huu wakati akiokota
kuni na kuiomba serikali kusaidia kuwaondoa Tembo hao.
Amesema
Vifo hivyo na majeruhi vimetokana na makundi ya Tembo yanayovinjari
Kijijini hapo nyakati za usiku huku kukiwa hakuna jitihada zozote
zinazochukuliwa na serikali katika kuwadhibiti wanyama hao wanaotoroka
kutoka hifadhi ya Tarangire na Manyara kusaka malisho.
Mwenyekiti
huyo aliwataja marehemu waliouawa na Tembo kwa nyakati tofauti kuwa ni
Janeth Silla,Mamalai Kakuyu, Lemomo Lenguriny, Kastuli Jumalei, Emanuel
Leroo na Ester Sindiyo wote wakazi wa Kijiji hicho.
Pia
aliwataja majeruhi wa tembo hao kuwa ni Lobulu Mollel, Julius Thobias
,Saiguran Mika, Mnyak Lenguriny,Mjomba Soingei bado amelazwa katika
hospital ya rufaa KCMC, Lobikyeki Sanare na Kalai Lomayani wote wakazi
wa Kijiji Cha Makuyuni na kwamba taarifa za matukio hayo wamekuwa
wakizitoa katika ngazi mbalimbali.
Naye
diwani wa kata hiyo Elius Odupoi aliwataka wananchi kuchukua tahadhali
ya kujilinda wenyewe na kuacha kutembea nyakati za usiku ikiwemo kufanya
shughuli za kijamii majira ya usiku.
"Watu
wetu wanauawa na Tembo na wengine wanajeruhiwa tunaendelea kuikumbusha
serikali iongeze nguvu ya kudhibiti Hawa Tembo ,na sisi wananchi
tupunguze kufanya shughuli zetu nyakati za usiku na suala la ulinzi
linaanza na sisi."alisema Diwani.
Mmoja
ya mwananchi wa Kijiji hicho,Peter Laisangai alimeiomba serikali
kuongeza fidia kwa wahanga wa wanyamapori kwani kiasi cha Sasa
kinachotolewa na serikali Cha sh.500,000 kwa aliyejeruhiwa na shilingi
1,000,000 kwa aliyefariki ni kidogo .
"Tunaiomba
serikali kupitia upya kiasi kinachotolewa kama kifuta jasho kwa
waathirika wa wanyamapori kwani hakiendani na thamani ya mwananchi
anayelinda rasilimali hizo."alisema Leisangai
Naye
afisa wanyamapori wilaya ya Monduli, Seraphino Mawanja aliyehudhuria
mazishi hayo alisema katika kipindi cha miaka miwili maeneo hayo
yamekuwa na changamoto kubwa ya ongezeko la Tembo ambao walihama kutoka
hifadhi ya Tarangire baada ya mvua nyingi kunyesha na maeneo yao kujaa
maji.
Alisema serikali imekuwa ikichukua hatua kadhaa kuwaondoa Tembo hao wanaovamia maeneo ya makazi kwa kuweka askari wa doria.
Hata
hivyo alisisitiza kuwa serikali inajitahidi kufidia wananchi
wanaoathiriwa na Tembo kwa kutoa kifuta jasho cha shilingi Milioni moja
kwa aliyeuawa na Tembo na sh. laki tano kwa majeruhi.
No comments :
Post a Comment