Thursday, January 28, 2021

TAKUKURU IMEWATAKA WANAHABARI KUONGEZA JUHUDI KUHAMASISHA JAMII KUKABILIANA NA RUSHWA

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brig.Jen John Mbungo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa TAKUKURU TV yenye lengo la kuwahabarisha watanzania kuhusu mapambano dhidi ya Rushwa.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brig.Jen John Mbungo akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Flaver Media Bw.John Bukuku katika hafla ya uzinduzi wa TAKUKURU TV yenye lengo la kuwahabarisha watanzania kuhusu mapambano dhidi ya Rushwa iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brig.Jen John Mbungo akimkabidhi cheti Mhariri wa Gazeti la Majira Bi.Stella katika hafla ya uzinduzi wa TAKUKURU TV yenye lengo la kuwahabarisha watanzania kuhusu mapambano dhidi ya Rushwa uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brig.Jen John Mbungo akimkabidhi cheti mwandishi wa habari wa Mwamba wa Habari Blog katika hafla ya uzinduzi wa TAKUKURU TV yenye lengo la kuwahabarisha watanzania kuhusu mapambano dhidi ya Rushwa uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Wanahabari wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa TAKUKURU TV yenye lengo la kuwahabarisha watanzania kuhusu mapambano dhidi ya Rushwa uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brig.Jen John Mbungo akipiga makofi katika hafla ya uzinduzi wa TAKUKURU TV yenye lengo la kuwahabarisha watanzania kuhusu mapambano dhidi ya Rushwa.

Gari la Matangazo ambalo litatumika katika utoaji elimu kuhusu mapambano dhidi ya Rushwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini, gari hilo lilizinduliwa katika hafla ya uzinduzi wa TAKUKURU TV yenye lengo la kuwahabarisha watanzania kuhusu mapambano dhidi ya Rushwa.

PICHA NA EMMANUEL MBATILO

******************************************

NA EMMANUEL MBATILO 

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU imewataka wanahabari kutumia vyema

na kwa usahihi kalamu zao katika kuhamasisha kuendelea kukabiliana na janga la Rushwa.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brig.Jen John Mbungo wakati akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa TAKUKURU TV yenye lengo la kuwahabarisha watanzania kuhusu mapambano dhidi ya Rushwa.

Mkurugenzi huyo wa TAKUKURU amesema ni vyema jamii ikaonyesha muamko wa kukabiliana na vitendo vya Rushwa kwa kuwa wamoja katika kudumisha amani ili kuchochea maendeleo ya nchi.

Awali akizungumza Mkurugenzi wa Elimu kwa umma TAKUKURU Joseph Mwaiswelo ametaja majukuu ambayo watayafanya kuwa ni pamoja na kuandaa mipango ya kuelimisha na kushirikisha vijana kwa makundi mbalimbali kwenye janmii.

Kwa upande wao baadhi ya wanahabri ambao wameshiriki katika hafla hiyo sambamba na kupata cheti cha kuhabarisha umma katika kutangaza na kuandika habari kuhusu Rushwa wameeleza kuwa wataendelea kunyosha ushirikiano katika mapambano dhidi ya Rushwa.

Katika hafla hiyo ya Takukuru wamehudhuria wanahabri na wakurugenzi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini ambapo wameendelea kuhamasishwa kuzitoa na kuzitangaza taarifa mbalimbali kuhusiana na rushwa ili kukabiliana na janga hilo na hivyo kuendeleza maendeleo kwa nchi.

 

No comments :

Post a Comment