Sunday, January 31, 2021

TADB YAWEZESHA WAFUGAJI KUPATA NG’OMBE WA KISASA WA MAZIWA


Meneja
wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya Kilimo (TADB) Jeremiah Mhada wa
kwanza kulia akimkabidhi hundi ya Sh Milioni 396 Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mashimba Ndaki kwa ajili ya wafugaji mkoani Tanga kupata mbegu ya
ng’ombe bora wa kisasa wa maziwa wakiwemo wafugaji 114 kupitia vyama vya
msingi 5 kupata mikopo ya ng’ombe wa kisasa wa kwanza kushoto
anayshuhudia ni Kaimu Msajili bodi ya maziwa Noely Byamungu

Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya Kilimo (TADB) Jeremiah Mhada wa
kwanza kulia akimkabidhi hundi ya Sh Milioni 396 Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mashimba Ndaki kwa ajili ya wafugaji mkoani Tanga kupata mbegu ya
ng’ombe bora wa kisasa wa maziwa wakiwemo wafugaji 114 kupitia vyama vya
msingi 5 kupata mikopo ya ng’ombe wa kisasa wa kwanza kushoto
anayshuhudia ni Kaimu Msajili bodi ya maziwa Noely Byamungu

Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya Kilimo (TADB) Jeremiah Mhada wa
kwanza kulia akimkabidhi hundi ya Sh Milioni 396 Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mashimba Ndaki kwa ajili ya wafugaji mkoani Tanga kupata mbegu ya
ng’ombe bora wa kisasa wa maziwa wakiwemo wafugaji 114 kupitia vyama vya
msingi 5 kupata mikopo ya ng’ombe wa kisasa wa pili kushoto
anayeshuhudia ni Kaimu Msajili bodi ya maziwa Noely Byamungu


Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya Kilimo (TADB) Jeremiah Mhada akizungumza wakati wa halfa hiyo

Sehemu
ya wafugaji wakimsikiliza Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya


Kilimo (TADB) Jeremiah Mhada akizungumza wakati wa halfa hiyo

BENKI
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imekwisha toa mikopo yenye
thamani ya Shilingi billioni 11.80 ili  kuwezesha mnyororo wa thamani wa
sekta ya maziwa kote nchini.

Pia imewezesha wafugaji Mkoani
Tanga kupata mbegu ya ng’ombe bora wa kisasa wa maziwa wakiwemo wafugaji
114 kupitia vyama vya msingi 5 kupata mikopo ya ng’ombe wa kisasa wenye
thamani ya Zaidi ya Tsh 396m.

Akizungumza katika hafla
iliyoandaliwa na shirika la kimataifa la Heifer,Meneja wa Kanda ya
Mashariki wa Benki ya Kilimo (TADB) Jeremiah Mhada alieleza umuhimu wa
ushirikiano wa wadau muhimu katika sekta ya mifugo ili kuongeza tija
nakuleta mapinduzi ya kweli katika sekta ya maziwa nchini.

Alisema 
kupitia mkopo huu, TADB imeweza kuwajengea wafugaji hao mabanda ya
kutunzia ng’ombe 25 na kupata mitamba ya kisasa ili wanufaike na
ufugajiwa ng’ombe wa maziwa ikiwemo kupatiwa mikopo naafuaa
itakayowawezesha kupata mbegu bora za ng’ombe wa maziwa.

 “TADB
ili kuhakikisha wafugaji wananufaika na sekta hii ya maziwa tuliingia
katika ushirikiano na shirika la kimataifa la Heifer International
kuhakikisha wafugaji wetu wanajengewa uwezo wa namna bora ya ufugaji wa
ng’ombe wa maziwa lakini pia kujiunga katika vikundi ili kuweza kupata
mikopo kwa urahisi.”Alisema

TADB imewezesha vyama vya msingivya
UWAMWA, CHAWAMU, UWAKO, UWAMKI na UWADAKI kuweza kupata jumla ya ng’ombe
wa kisasa 156 kwa wafugaji 121 ikiwemo wanawake 39 pamoja na
kuwawezesha kupata mkopo huo wafugaji hao tayari wana soko la kuuza
maziwa yao.

“Kwa hapa Tanga wataweza kuuza kwa kampuni ya Tanga
Fresh ambayo nayo TADB imekwisha iwezesha katika kumudu kuweza kununua
maziwa kutoka kwa wafugaji hawa wadogowadogo.” Alisisitiza Mhada.

Kabla
ya kufanya makabidhiano hayo,TADB kwakushirikiananaShirika la kimataifa
la Heifer International waliendesha mafunzo kwa viongozi wa vyama vya
ushirika 26 ambao walijengewa uwezo kwenye namna ya usimamizi bora wa
biashara, usimamizi wa fedha, utunzaji wa kumbukumbu, utunzajiwa
kumbukumbu na uongozi bora.

“Ufugaji ili uwe na tija nilazima
wafugaji wajengewe uwezo na ni muhimu kufahamu namna ya kusimamia
fedha, utunzaji wa kumbukumbu,uongozi bora na masuala mengine ya
usimamizi wa biashara kwa kuwa na uwezo huu, mfugaji anaweza kuona namna
anavyonufaika na mkopo na hata kuweza kufahamu kipato chake.”Aliongezea
Mhada.

Alisema Wafugaji wadogo kupitia TADB wanaendelea
kunufaika na fursa zilizopo kupitia benki ya kilimo na pia kupitia
ushirikiano huo wa TADB nashirika la kimataifa la Heifer.
 
Serikali
imeainisha sekta ya maziwa kama moja ya sekta muhimu katika kuchochea
uwekezaji katika viwanda jambo ambalo TADB inawawezesha wawekezaji kama
kampuni za Tanga Fresh, Kahama Fresh, Njombe Milk na viwanda vingine
katika maeneo mbalimbali nchini.

Aliongeza kwamba kupitia
uwekezaji katika mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo, pia kama Taifa
wanaweza kujihakikishia upatikanaji na usalama wachakula,lishe bora na
kipato kwa wafugajina pia kuongezapato la Taifa.

Mhada alisema
sekta  ya maziwa nchini inachangia asilimia 1.2% yapato la Taifa huku
akieleza ili kuhakikisha wanaongeza kipato kwa wafugaji wadogo wadogo
ambao kupitia shughuli hizi za ufugaji huchangia pato la Taifa.Alisema
wamewezesha kupata mitamba ya kisasa na kuwaunganisha na masoko ili
kuongeza thamani na kuchochea ongezauzalishaji wa mazi wa nchini.

No comments :

Post a Comment