Waziri wa Afya,
Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima akiongea
na Viongozi wa Vyama,Bodi na Mabaraza ya kitaaluma vilivyopo chini ya
sekta ya afya nchini
Naibu Waziri Dkt. Godwin Mollel akiongea wakati wa kikao kazi na
mabaraza,bodi na vyama vya kitaaluma kwenye ukumbi wa hospitali ya
Benjamin Mkapa
Baadhi wa watendaji
wa wizara ya afya makao makuu wakifuatilia mkutano huo ambao unajadili
maadili na weledi wa wanataaluma kwenye vituo vya vya kutolea huduma
nchini
Washiriki wa kikao kazi hicho kwenye ukumbi wa hospitali ya Benjamin Mkapa
*********************************************
Na. Catherine Sungura,WAMJW-Dodoma
Vyama, Mabaraza
pamoja na bodi za kitaaluma nchini vimetakiwa kudhibiti maadili na
weledi katika utendaji kwa watumishi wa sekta ya afya nchini ili
kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.
Hayo yamesemwa
leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.
Dorothy Gwajima wakati wa kikao na viongozi hao kwenye ukumbi wa
hospitali ya Benjamin Mkapa jijiji Dodoma.
Dkt.Gwajima
amesema kuwa vyama, bodi na mabaraza ya kitaaluma ndio wasimamizi wakuu
na wadhibiti wa maadili na weledi ambapo wananchi bado wanakutana na
changamoto nyingi za maadili na weledi wakati wa upataji huduma za
afya.
“Kwenye Ilani ya
Chama cha Mapinduzi ya uchaguzi kurasa 137 imeandikwa kushirikiana na
vyama vya kitaaluma vya kada ya afya katika kusimamia uzingatiaji wa
maadili na weledi katika utendaji wa watumishi hilo ndio tunalotekeleza.
“Amesisitiza Dkt. Gwajima.
Amesema
wanapofanya ziara kwenye mikoa mbalimbali wanakutana na kero zitokanazo
na kufifia kwa maadili na weledi wa utendaji, huku akiweka wazi kuwa,
haya yote yanadhibitiwa na vyama, bodi na mabaraza ya kitaaluma.
“Ili tuweze
kuhuisha hayo yote, lazima tukae pamoja na kuangalia mifumo yao ya
utendaji kazi ukoje hadi unatoa mianya ya baadhi ya wanataaluma kukosa
maadili na kuleta malalamiko mengi kutoka kwa wananchi?,Aliuliza Dkt.
Gwajima
Aidha, Dkt.
Gwajima amesema kutokana na malalamiko hayo inafanya kuonekana kukosa
meno ya vyama hivyo vya kitaaluma, hivyo kikao hicho kikubwa ni kuambina
ukweli na kuwakumbusha majukumu yao na wafahamu kuna tatizo kwa
wanataaluma wao ndio mana hawashtuki na hata wengine kuvunja maadili
bila kujali kama kuna mabaraza ya kitaaluma na kubadilika ili kuondoa
kero kwa wananchi.
Kwa upande wa
kuwa na mwamvuli mmoja wa mabaraza yote ni kwamba itasaidia kuwa na timu
moja na matumizi ya fedha ya kuendesha mabaraza yote yatapungua na
kuongeza ufanisi na tija ya wataalam wengine ili wakae kwenye maadili.
Naye Naibu Waziri
Dkt. Godwin Mollel amewataka viongozi hao kuwajibika ili kuondoa
matatizo ambayo ama wao kama mabaraza hawayaoni au yanaonwa na viongozi
wa wilaya eneo husika.
Dkt. Mollel
aliendelea kusema kuwa, wataalamu wengi hivi sasa hawafanyi kazi kwa
kuzingatia maadili na hivyo kusababisha makosa mengi ya kitaaluma
yanafanyika kwenye vituo vya kutolea huduma na wananchi wengi kupoteza
maisha na wengine kupata athari kwenye jamii.
“Tunakuta makosa
kwenye taaluma mfano dawa zinaibiwa lakini wewe mwenye baraza lako na
unasimamia maadili hulioni hili hivi hujioni kwamba na wewe unatakiwa
kuadhibiwa? Aliuliza Dkt.Mollel
Hatahivyo
amewataka viongozi hao kujitafakari kama wanatosha kwenye mabaraza yao
kama wanashindwa wao kugundua matatizo yaliyopo chini kwani wanakuwa
wameshindwa kusimamia na kufanya kazi zao vizuri kwa kutoa adhabu kwa
wanaofanya makosa na kusababisha matatizo kwa wananchi.
No comments :
Post a Comment