Charles James, Michuzi TV
SERIKALI imeshuhudia utiaji saini wa mikataba ya kupeleka mawasiliano vijijini awamu ya tano baina ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF) na
makampuni ya simu za mkononi.Hafla hiyo ya utiaji saini makubaliano hayo imefanyika jijini Dodoma leo na kushuhudiwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile.
Akizungumzia makubaliano hayo Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Justina Mashiba amesema katika mradi wa Mawasiliano Vijijini awamu ya tano jumla ya kata 61 zenye vijijini 173 na wakazi 728,840 zitafikishiwa mawasiliano huku alisema kwa mujibu wa mkataba huo hadi kufikia Oktoba mwaka huu mradi unatakiwa uwe umekamilika.
Kwa upande wake Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk Faustine Ndugulile ameyaonya makampuni ya simu za mkononi juu ya utoaji wa siri za wateja huku akisema kuwa kwa kampuni itakayotolewa malalamiko ya kufanya hivyo itachukuliwa hatua kali za kisheria.
Amesema Wizara hiyo itahakikisha inatunga sheria ya kuwalinda wateja wa simu za mkononi ili kuondoa tabia hiyo ya kutoa siri zao.
" Niwaonye makampuni yanayotoa taarifa za siri za wateja, tutawachukulia hatua wote kwa sababu kufanya hivyo ni kinyume na sheria hivyo kampuni itakayobainika itachukuliwa hatua.
Niyatake makampuni ya mawasiliano kusoma sheria na kuielewa ili waweze kufanya kazi kwa mujibu wa sheria. Lazima tuhakikishe tunapeleka mawasiliano huko maeneo ya mipakani badala ya kufikiria miji ya kibiashara tu,lakini pia tunapokuwa katika maeneo hayo tukaribishwe na mitandao ya kwetu na siyo ya nchi jirani," Amesema Naibu Waziri Dk Ndugulile.
No comments :
Post a Comment