Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyosambaa katika Mitandao ya kijamii juu ya BRELA kukimbiza wawekezaji kutokana na changamoto za Mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS).
Wakala inatambua dhamana iliyopewa na serikali ikiwa ni pamoja nakuhakikisha shughuli za Uwekezaji zinaongezeka nchini, hivyoinaendelea kufanyia kazi changamoto mbalimbali ambazo zimekua zikionekana kuwanikikwazo katika urasimishaji wa biashara kupitia Mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao.Ifahamike kwamba, mwezi Mei 2020, BRELA kwa kushirikiana na wataalam wa mifumo toka Taasisi mbalimbaliza serikali ilianza rasmi kubadilisha na kuboresha mfumo (System Re-designing) kwa kuzingatia changamoto zilizopo katika mfumo unaotumika hivi sasa.
Mfumo huo kwa sasa upo katika hatua za majaribiona utakapo kuwa tayari utakabidhiwa kwa ajili yakuanzakutumikarasmihuku ukisimamiwa na wataalam wazawa tofauti na mfumo wa sasa unaosimamiwa na Mzabuni kutoka nje ya nchi.Kukamilika kwa Mfumo huo kutaweza kutatua changamoto zilizopo ikiwa ni pamoja na Maombi kupokelewa na kufanyiwa kazi na Ofisa mmoja, Ombi kufanyiwa kazi kwa kuzingatia ombi lililofika awali (firstcome,first served), kuendelea kuunganisha Mfumo wa BRELA na mifumo ya taasisi nyingine kama Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA),Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA), Benki, Uhamiaji na Mamlaka za utoaji Leseni katika Halmashauri.
Lengo kuu ni kutengeneza mazingira rafiki na wezeshi sio tu kwa wawekezaji bali wafanyabiashara wote.Aidha, katika kuhakikisha kwamba katika kipindi hiki Wadau wa BRELA wanapata huduma nzuri, Wakala imeanzishaKituo cha Miito na Huduma kwa wateja. Kituo hiki kazi yake kuu ni kutoa usaidizi wa haraka kwa Wateja wetu wanapokwama wakati wa urasimishaji wa Biashara zao.
Ni vyemaumma ufahamu kwamba, muda wa usajili wa Jinala biashara ni siku moja(1)na si zaidi yasiku tatu(3)za kazi, Usajili wa kampuni ni siku tatu(3)na si zaidi ya siku tano(5)za kazi, Usajili wa Alama za Biasharana huduma ni kipindi cha siku tisini (90) (kutokana na takwa la kisheria), maombi ya kupataHataza ni siku mia moja na ishirini (120)(kutokana na takwa la kisheria),kupata Leseni ya Kiwanda au Leseni ya Biashara kundi A ni siku moja(1)na si zaidi ya siku tatu(3)za kazi.JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA VIWANDA NA BIASHARAWAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA LESENI
Baada ya kipindi hicho kupita kama usajili haujakamilika Mtejaawasiliane na kituo cha huduma kwa Wateja kupitia namba +255 (0) 222 212 800 au kwa barua pepe maoni@brela.go.tzkwa ajili ya usaidizi wa haraka.
Hivyo basi,Wakala inawataka wadau wake kufuata taratibu za usajili ikiwa ni pamoja na ujazaji wa taarifa kwa makini na uwekaji wa viambatanisho sahihi ili kuepusha kuchelewa kwa kukamilika kwa usajili.BRELA wakati wote tunapokea maoni ya wadau kwa lengo la kuboresha sio tu mifumo bali pia uendeshaji wa Taasisi yetu“Tunaipa utu wa kisheria biashara yako”
Imetolewa na:
KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
WAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA LESENI
No comments :
Post a Comment