RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiondoka katika viwanja
vya ukumbi wa mkutano wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini
Zanzibar baada ya kumaliza mazungumzo yake na Walimu na Wadau wa Elimu
Zanzibar na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja
Mhe.Idrisa Kitwana Mustafa na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said.(Picha na Ikulu)
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya
Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said akizungumza kabla ya kumkaribisha
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein
Ali Mwinyi, kuzungumza na Walimu na Wadau wa Elimu Zanzibar mkutano
uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini
Zanzibar.(Picha na Ikulu)
WADAU wa Elimu Zanzibar
wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi, wakati wa mkutano huo wa
kuzungumzia hali ya Elimu Zanzibar,uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh
Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein
Ali Mwinyi akifuatilia michango ya Wadau wa Elimu Zanzibar uliofanyika
katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar na
(kulia kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi
Mhandisi Zena Ahmed Said na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Walimu na
Wadau wa Elimu Zanzibar, baada ya kupokea changamoto zinazowakabili
katika Sekta ya Elimu Zanzibar, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa
Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu) 
/MDAU wa Elimu kutoka Chuo cha
Mwalimu Nyerere Tawi la Zanzibar Bi. Rose Mbwete akichangia wakati wa
mkutano huo na Wadau wa Elimu Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa
Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
MWENYEKITI wa Chama Cha Walimu Zanzibar (ZATU) Ndg.Salum Ali Salim akiwasilisha Changamoto za Elimu kwa Walimu Zanzibar, wakati wa mkutano wao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
No comments :
Post a Comment