Tuesday, January 26, 2021

MAZAO YA MBOGA ZA ASILI MBIONI KUTOWEKA AFRIKA - MIZENGO PINDA


Na Woinde Shizza, Michuzi TV- ARUSHA
WAZIRI mkuu mstaafu Mizengo Pinda amesema pamoja na Afrika kuwa na
zaidi ya mboga za asili 400, mazao hayo yapo mbioni kutoweka huku
Tanzania ikikabiliwa na utapiamlo kutokana na kula chakula kisichokuwa
na viini lishe bora.

Waziri Punda aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa kimataifa
uliowakutanisha wadau wa mazao ya bustani jijini Arusha,  alisema
kuwa takwimu za utafiti wa mwaka 2018 zinaonyesha hali ya utapiamlo
nchini hapa  ni mbaya kutokana na baadhi ya watu kutokula chakula
chenye viini lishe bora.

“Hali  utapiamlo nchini ni mbaya kulingana na takwimu za utafiti wa hali ya lishe ya mwaka 2018 ambapo imeonyesha watoto wengi ndio wanaathiriwa zaidi na ugonjwa huo pamoja na wanawake kuwa na uzito unaozidi ikiwa hali hii imechangia kuongezeka kwa gharama ya matibabu kwa familia na serikali hivyo kuna hitajika msisitizo wa uzalishaji wa mboga zenye asili ya kiafrika ili kusaidia kupunguza utapiamlo barani Afrika.”Alisema.

"Takwimu zinaonyesha hali ya utapiamlo kwa upande wa watoto chini ya
miaka mitano milioni 3 wamedumaa,milioni 1.3 wanauzito pungufu,milioni
5 wanaupungufu wa damu na wengine milion 3 wanaupungufu wa vitamini A
ikiwa asilimia 32 ya wanawake(14-49) wanatatizo la uzito
uliozidi."Alisema Pinda.

Alisema athari ya utapiamlo ni kubwa katika jamii ikiwemo
vifo, kupunguza ufahamu na ubunifu, madini chuma ikiwa wanawake zaidi
ya elfu 60 hupoteza maisha kwa mwaka kutokana na upungufu wa damu
kwani taarifa za mwaka 2019 onaonyesha kuwa Tanzania inatumia
takribani sh.bilioni 454 kwa mwaka kwa ajili ya kugharamia magonjwa ya
kisukari,moyo,figo,ini ,kinywa pamoja na uoni hafifu na usikivu.

"Mazao ya mbogamboga pia ni fursa kubwa sana ya kibiashara katika
ngazi ha kaya na Taifa kwa ujumla ikiwa serikali inaendelea na
uhamasishaji wa kilimo cha mazao ya lishe ili kupunguza udumavu kutoka
asilimia 32 hadi 24 pamoja na ukondefu kwa kuendelea kuwa chini ya
asilimia 5 kiwango ambacho kimewekwa na shirika la afya."Alisema
Pinda.

Aidha alisema kuwa kazi ya kuhamasisha uzalishaji na matumizi ya mazao
ya mboga yenye asili ya kiafrika si kazi ya serikali tu bali ni kazi
ya wadau wote wakiwemo ,watafiti ,wakulima,wafanyabiashara na sekta ya
usafirishaji,uuzaji wa mazao  ghafi na usindikaji  wote wakiungana
watafanya kazi nzuri.

"Hivyo wadau wa Maendeleo wa sekta binafsi na ile ya serikali kufanya
Kila linalowezekana kuhakikisha mazao haya yanapewa kipaumbele kwa
kuweka nguvu nyingi Katika utafiti na hasa Katika maeneo ya ukusanyaji
,utunzaji na uboreshaji wa mbegu za mazao ikiwa ni pamoja na ulimaji
bora na matumizi yenye kuimarisha lishe na afya ya mlaji."Alisema.

Naye mkurugenzi wa kanda ya mashariki na kusini mwa afrika Kituo mboga
duniani (worldveg) Dkt.Gabriel Rugalema alisema kuwa mkutano huu
utasaidia kuhakikisha wanajenga mkakati utakao hamasisha ongezeko la
mazao haya pamoja na namna ya kuyatunza kwa ajili ya  vizazi vijavyo.

"Ukiangalia mboga za asili ziko mbioni kupotea kwani mazao mengi
tunaletewa kutoka nje pamoja na kuwa na mboga za kiasili tumekuwa bara
la kupokea mbegu kutoka nje ambazo zinaharibu udongo na afya ya
binadamu kutokana na madawa yanayo nyunyuziwa kwenya mboga
hizo." Alisema Rugalema.

Rugalema alisema suala hilo la kuzalisha wasicho kula halivumiliki,
hivyo ni vyema mazao ya mboga za kiasili yakawe mazao ya kibiashara
kwani itafika mahali mchicha na mgagani zitabaki kusimuliwa kwenye
vitabu wasipoweka mikakati ya pamoja ili kulinda mazao hayo.

Alisema kuwa zaidi ya watu 200 wameshiriki moja kwa moja mkutano huu
na watu mengine 1000 wameshiriki kwa njia ya mtandao hiyo inatokana na
kuwepo na mlipuko wa Mara yapili ya ugonjwa wa Covid 19.

Naye mchumi wa baraza la biashara la afrika mashariki (EABC)  Adrian
Njau aliwataka watu  wajikite kwenye mazao yao wenyewe kuliko
kutegemea  mazao  ambayo yanatoka nje ,huku akiwasisitiza wataalam
waendelee  kufanya utafiti zaidi wa mboga za ndani.

 

No comments :

Post a Comment