Waziri
mkuu mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Agri Thamani Foundation
Mizengo Pinda akizungumza na waandishi wa habari Jana Mara baada ya
kufungua mkutano wa duniani wa kujadiliana jinsi ya kuhamasisha na
kuongeza uzalishaji wa mazao ya mboga hasa yenye asili ya kiafrika
inayofanyika jijini hapa ambapo aliwasisitiza wanahabari kutumia kalama
zao kuelimisha wananchi namna ya kupambana na tatizo la utapia mlo
kupitia kilimo cha mboga na matunda.
mtafiti
wa mazao ya mboga kutoka kituo Cha kimataifa cha utafiti wa mazao ya
mboga ya asili ya kiafrika (world vegetable center ) Inviolate Dominick
akitoa maelekezo ya umuhimu wa viungo kwa ajili ya kuboresha
lishe,afya ,na hata kibiashara kwa mmoja ya mshiriki wa mkutano wa
duniani wa kujadiliana jinsi ya kuhamasisha na kuongeza uzalishaji wa
mazao ya mboga hasa yenye asili ya kiafrika inayofanyika jijini hapa.
(Picha na Woinde Shizza , ARUSHA)
Na Woinde Shizza , Michuzi Tv -Arusha
KUFUATANA
na takwimu za Shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa (FAO)
limebaini kuwa takribani watu milioni 821 wanakabiliwa na matatizo ya
utapiamlo yanayotokana na kula vyakula visichokuwa na viini lishe bora.
Hayo
yalibainishwa na waziri Mkuu mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa
shirika la agri thamani foundation Mizengo Pinda alipokuwa akifungua
mkutano wa kimataifa unaoangazia mazao ya kiasili ya afrika
inayofanyika mkoani hapa Katika ukumbi wa hotel ya gran melia ambapo
alisema kuwa kuwa upande wa hapa nchini Tanzania Hali ya utapiamlo ni
mbaya kulingana na takwimu za utafiti wa hali lishe ya mwaka 2018
ambazo zinaonyesha watoto wengi ndio wanaathieriwa sana na tatizo hilo.
Alisema
kuwa kulingana na takwimu hizo zinaonyesha watoto wenye umri kuanzia
miaka 0 - 5 milioni tatu wamedumaa,watoto wa miaka 0-5 milioni 1.3
wanauzito pungufu, watoto wenye umri wa miaka 0-5 milioni tano
wanaupungufu wa Damu,, watoto wenye umri huohuo 0-5 milioni tatu
wanaupungufu wa vitamin A na asilimia 32 ya wanawake wenye umri wa miaka
14 -49 wanatatizo la uzito uliozidi.
Alibainisha
baadhi ya adhari ya utapia mlo ni pamoja na udumavu ambao una athari
Katika makuzi na maendeleo ya watoto kwa sababu hupunguza ufahamu na
ubunifu kati ya asilimia 30 hadi 40 ambapo hali hiyo huadhiri uwezo wa
mtoto kufundishika ,kuelekezwa na kushusha ufaulu, na pia utapia mlo
unaongeza magonjwa na vifo vya watoto na akina mama.
"Miongoni
mwa asilimia 50 ya magonjwa ambayo husababisha vifo vya watoto wenye
umri Chini ya miaka mitano vinavyosababishwa na utapiamlo ,pia wanawake
takribani 60,000 hufariki kila mwaka kutokana na matatizo ya upungufu wa
damu yanayotokana na tatizo la upungufu wa damu linatokana na upungufu
wa madini china.
Aidha
alisema kuwa mazao ya mboga ni muhimu kwenye afya lishe kwani utafiti
wa kitaalam unaonyesha kuwa mboga za asili ya afrika zina viwango
vikubwa vya viini lishe ukilinganisha na mboga zingine kutoka mataifa ya
nje ya bara la Africa ambapo alibainisha kuwa watu wa nje ya afrika
wanayaita mazao haya kuwa ni “super foods” yaani vyakula venye viini
lishe bora kabisa.
"Afrika
tunazaidi ya aina 400 za mazao ya mboga za kiasili lakini yale
yanayotumika Kama chakula ni machache Sana na yale yanayotumika
kibiashara ni machache zaidi ,huu ni urithi wetu wa mazao haya nilazima
tuyatunze na kuyaenzi kwa sababu mbalimbali moja wapo ikiwa mazao ya
mboga ni muhimu Sana kwa afya lishe ,pia kwa ajili ya kutunza bioanuai
yetu isipotee
Alisema
mbali na mazao ya mboga kusaidia kupunguza utapia mlo pia ni fursa
kubwa Sana ya kibiashara Katika ngazi ya kaya na taifa kwa ujumla ,kwa
afrika na Tanzania ambapo ukienda sokoni utaona kuwa mboga hizi zimekuwa
njia moja wapo ya kujipatia kipato hasa kwa kina mama na vijana .
"Tanzania
Kutambua ukubwa wa tatizo hili imeamua kupitia ilani ya uchaguzi ya
chama tawala CCM 2020-2025 kuweka uzito mkubwa kwa kuahidi kuhamasisha
kilimo cha mazao lishe Ili kupunguza udumavu kutoka Asilimia 32 hadi
24,pamoja na kupunguza ukondefu Ili kuendelea kuwa chini ya Asilimia 5
kiwango ambavyo kimewekwa na dunia, pia kuongeza uzalishaji wa mazao ya
bustani kutoka Tani 7,230,217 hadi tani 14,600,000ifikapo mwaka 2025 na
Ili kufikia malengo haya tuneainisha mambo kadhaa ikiwemo kujengea uwezo
wa taasisi za ndani za serikali na binafsi za ithibati Ili kupunguza
gharama za ithibati za mazao yanayosafirishwa nje hasa mazao ya bustani
na mboga ambavyo wawekezaji wake wakuu ni wanawake na vijana
"alibainisha Pinda
Pinda
alisema kuwa kazi ya kuhamasisha uzalishaji na matumizi ya mazao ya
mboga yenye asili ya kiafrika si kazi ya serikali tu bali ni kazi ya
wadau wote wakiwemo ,watafiti ,wakulima,wafanyabiashara na sekta ya
usafirishaji,uuzaji wa mazao ghafi na usindikaji wote wakiungana
watafanya kazi nzuri ,aidha alitoa wito kwa wadau wa Maendeleo wa sekta
binafsi na ile ya serikali kufanya Kila linalowezekana Kuhakikisha mazao
haya yanapewa kipaumbele,pia niasisitize ni vyema tukaweka nguvu nyingi
katika utafiti na hasa Katika maeneo ya ukusanyaji ,utunzaji na
uboreshaji wa mbegu za mazao haya ulimaji bora na matumizi yenye
kuimarisha lishe na afya ya mlaji
Naye
mkurugenzi wa kanda ya mashariki na kusini mwa afrika ,world vegetable
center Dkt.Gabriel Rugalema alisema kuwa mkutano huo utasaidia
kuhakikisha wanajenga mkakati utakao hamasisha ongezeko la mazao haya
pamoja na namna ya kuyatunza
Alisema
kuwa zaidi ya watu 200 wameshiriki moja kwa moja mkutano huu na watu
mengine 1000 wameshiriki kwa njia ya mtandao hiyo inatokana na kuwepo na
mlipuko wa Mara yapili ya ugonjwa wa Covid 19.
Naye
mchumi wa baraza la biashara la afrika mashariki (EABC) Adrian Njau
aliwataka watu wajikite kwenye mazao yetu wenyewe kuliko kutegemea
mazao ambayo yanatoka nje ,huku akiwasisitiza wataalam waendelee
kufanya utafiti zaidi wa mboga za ndani.
No comments :
Post a Comment