Friday, January 29, 2021

KAMATI YA BAJETI YA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR YAKUTANA NA UONGOZI WA OFISI YA RAIS FEDHA NA MIPANGO

Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Mh. Saada Mkuya Salum akihoji kitu wakati  kamati yake ilipokutana na Uongozi wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Ofisini kwao Vuga Mjini Zanzibar (kulia) Waziri ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango (Tehema) Rashid Said Rashid akieleza namna walivyojipanga kuhakikisho kodi zote zinalipwa kwa kutumia mtandao.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali akiieleza Kamati ya Bajeti ya Bazara la Wawakilishi mikakati waliyoandaa kuhakikisha Zanzibar Haitegemei Utalii tu kukuza uchumi wake.  

Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki ambae pia ni mjumbe wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Suleiman Haroub Suleiman akiuliza swali wakati kamati hiyo ilipokutana na Uongozi wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango. Baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar wakiandika maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi walipofika Ofisini kwao Vuga.

Picha na Makame Mshenga.

 

No comments :

Post a Comment