Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja, leo Januari 14, 2021 amekagua kituo cha kupoza umeme cha Mpomvu kilichopo Geita.
Ziara hiyo ni maandalizi ya Uzinduzi wa mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 220 kutoka Bulyanhulu hadi Geita ambao unatarajiwa kuzinduliwa rasmi hivi karibuni na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika ziara hiyo aliambatana na Kamishna Msaidizi wa umeme Mhandisi. Innocent luoga, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka pamoja na watumishi mbalimbali wa Wizara ya Nishati na TANESCO.
No comments :
Post a Comment