Tuesday, December 22, 2020

WAZIRI UMMY MWALIMU AJITAMBULISHA KWA RAIS WA ZANZIBAR


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa  Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi Ikulu Zanzibar mara baada ya kufanya mazungumzo  na Rais wa Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa  Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi Ikulu Zanzibar mara baada ya kufanya mazungumzo  na Rais wa Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha. Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Khalid Salum Mohammed (kulia) na Balozi Mbarouk Mbarouk Mkurugenzi Idara ya Muungano.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa  Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na  Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Maalim Seif Shariff Hamad mara baada ya mazungumzo  hii leo Visiwani Zanzibar, Waziri Mwalimu yuko Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa  Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu akiteta jambo na  Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Maalim Seif Shariff Hamad mara baada ya mazungumzo  baina yao hii leo Visiwani Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa  Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu akiteta jambo na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi Ikulu Zanzibar. Waziri Ummy Mwalimu yuko visiwani Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha.

*******************************************

Na Lulu Mussa

Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Ummy Mwalimu hii leo amefanya ziara ya kikazi visiwani Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha.

Waziri Ummy amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi Ikulu Zanzibar. Katika mazungumzo yao Mhe. Mwalimu amesema kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Zanzibar amedhamiria kuendeleza jitihada za kutatua changamoto za Muungano zilizobakia.

“Mhe. Rais nikuhakikishie kuwa nitafanya kazi kwa karibu sana na Mhe. Khalid Waziri mwenzangu kuhakikisha hoja ambazo bado hazijapatiwa ufumbuzi zinafanyiwa kazi na mwanzoni mwa mwezi Januari tunategemea kuwa na kikao cha pamoja baina yetu” Alisisitiza Mhe. Ummy.

Kwa upande wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amempongeza Mhe. Ummy Mwalimu wa kuteuliwa tena kuwa Waziri na kusisitiza kuwa Serikali yake itampa ushirikiano katika kuratibu masuala ya Muungano.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy Mwalimu amefanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharrif Hamad Chukwani Zanzibar.

Mhe. Hamad amesisitiza umuhimu wa Wizara zenye hoja za Muungano kukutana na kutafuta suluhu ya mapema na kuhamasisha  Wizara zisizo na hoja kukutana pia kwa lengo la kudumisha undugu baina ya  Tanzania bara na Tanzania Zanzibar.

“Nashauri na kusisitiza Wizara zinazoshabihiana zikutane na kuhakikisha hoja zinazopatiwa ufumbuzi zitekelezwe ipasavyo” alisisitiza Maalimu Seif Sharif Hamad.

Waziri Ummy Mwalimu yuko visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na hapo kesho atatembelea miradi ya Muungano inayotekelezwa pande zote mbili.

 

No comments :

Post a Comment