Tuesday, December 22, 2020

TPSF INA MCHANGO MKUBWA KWA MAENDELEO YA TAIFA-MAJALIWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Desemba 22, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuui) Baadhi ya washiriki wa kikao kati ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na viongozi wa Taasisi ya  Sekta Binafsi Tanzania (TPSF)  wakimsikiliza Mheshimiwa Waziri Mkuu wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Ofisi  Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Desemba 22, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

*****************************************

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) ndicho chombo

muhimu na chenye mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya kiuchumi Tanzania.

Ameyasema hayo leo (Jumanne, Desemba 22, 2020) alipokutana na Bodi mpya ya taasisi hiyo katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.

“Sisi Serikali tunapofurahi na kuwaambia Watanzania kwamba nchi yetu imeingia kwenye uchumi wa kati, hatuachi kuzungumzia namna ambavyo sekta binafsi ilivyoshiriki kiiamilifu kuleta mabadiliko.”

Kikao hicho ambacho ni uetekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipozindua Bunge la 12, jijini Dodoma, kuhusu ushirikiano kati ya Serikali na TPSF.

“Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi hii na kwenye changamoto tutahakikisha tunazipatia ufumbuzi kwa pamoja. Serikali inaimani kubwa na Taasisi hii ya Sekta Binafsi Tanzania.”

Kwa upande wao viongozi wa taasisi hiyo wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa ushirikiano inaowapatia ambao unawawezesha kutekeleza majukumu yao kwa urahisi na ufanisi mkubwa.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo, Waziri wa Viwanda na Biashara Geofrey Mwambe na watendaji wa taasisi za Serikali wanaohusika na usimamizi na uratibu wa maendeleo ya sekta binafsi.

 

No comments :

Post a Comment