Sunday, December 6, 2020

WAZIRI MKUU MAJALIWA AIPONGEZA BRELA


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akisoma Hotuba ya ufunguzi wa Maonesho ya 5 ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania katika Viwanja vya Mwl. Nyerere (Sabasaba), Dar es Salaam leo Desemba 04, 2020.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akiangalia vipeperushi vya Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) alipofika katika meza ya Wakala katika Kliniki ya Biashara mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Mwl. Nyerere (Sabasaba), Dar es salaam kwa ajili ya ufunguzi wa Maonesho ya 5 ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania ) leo Desemba 04, 2020.

Mkurugezi wa Idara ya Leseni kutoka Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Andrew Mkapa akifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa wakati ufunguzi wa Maonesho ya 5 ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania katika Viwanja vya Mwl. Nyerere (Sabasaba), Dar es Salaam leo Desemba 04, 2020.

***********************************

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ameipongeza

Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kwa utendaji wake wa kazi.

Mhe. Majaliwa ameyasema hayo leo Desemba 4, 2020 alipofika kwenye Banda la BRELA katika Maonesho ya 5 ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. Nyerere (Sabasaba) Jijini Dar es Salaamu¬.

“Nimefurahi kuwaona BRELA wapo hapa na nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya taarifa zenu tunazipata”. alisema Mhe. Majaliwa.

Naye Msaidizi wa Usajili Mwandamizi wa BRELA, Bw. Gabriel Girangay amesema kwamba, lengo kuu la kushiriki katika Maonesho hayo ni kutoa elimu na hamasa kwa Washiriki kuhusu Usajili wa Viwanda.

“Sisi kama BRELA hii kwetu ni fursa ya kuwafikia wadau wetu, moja ni kuwapa elimu juu ya Huduma tunazotoa, pili ni kutaka kuwahamasisha wadau juu ya Usajili wa Viwanda na mwisho ni kukutana na kutatua changamoto za wadau wetu papo kwa hapo pindi wanapofika katika Banda letu”. Alisema Bw. Girangay.

Maonesho ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yanafanyika mwaka huu kwa awamu ya tano tangu kuanzishwa kwake mwaka 2016 kwa lengo la kuhamasisha ukuaji wa Viwanda Tanzania. Ambapo yalianza Desemba 3 na yanatarajiwa kufikia tamati Desemba 9, 2020.

 

No comments :

Post a Comment