Sunday, December 6, 2020

JAMII YASHAURIWA KUNYWA MAZIWA KWA WINGI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel akizungumza katika bonanza la maziwa lenye lengo la kuhamasisha jamii kutumia maziwa kwa wingi.  Washiriki wa mbio katika Bonanza la Maziwa wakifurahia unywaji wa maziwa baada ya kumaliza mbio zenye lengo la kuhamasisha unywaji wa maziwa kwa wingi.

Balozi wa Maziwa ya Asasi ambaye pia niMsanii wa Bongo Fleva Shetta akizungumza katika Bonanza la Maziwa lenye lengo la kuhamasisha unywaji wa maziwa kwa wingi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel akiongoza mbio katika bonanza la maziwa lenye lengo la kuhamasisha jamii kutumia maziwa kwa wingi.Balozi wa Kampuni ya Maziwa ya Tanga Fresh Dkt. Issack Maro akizungumza katika Bonanza la Maziwa lenye lengo la kuhamasisha jamii kupendelea kutumia maziwa kwa wingi. Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Godwin Gondwe akizungumza katika Bonanza la Maziwa lenye lengo la kuhamasisha jamii kupendelea kutumia Maziwa kwa wingi. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Ludovick Nduhiye akizungumza katika katika Bonanza la Maziwa lenye lengo la kuhamasisha jamii kupendelea kutumia Maziwa kwa wingi. Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi Latifa Khamis akizungumza katika Bonanza la Maziwa lenye lengo la kuhamasisha jamii kupendelea kutumia Maziwa kwa wingi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel akiangalia baadhi ya bidhaa zilizozalishwa hapa nchini katika Maonesho ya 5 ya bidhaa za viwanda Tanzania yanayoendelea katika Viwanja vya Maonesho vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

************************************

NA EMMANUEL MBATILO

Mpaka sasa kuna Viwanda 99 vya Maziwa nchini na maziwa ambayo yanazalishwa sasa kwa mwaka 2020 yamefikia lita Bilioni 3.01.

Ameyasema hayo leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel katika bonanza la Maziwa lenye lengo la kuhamasisha unywaji wa Maziwa nchini.

Akizungumza katika bonanza hilo Prof.Elisante amesema uchakataji wa maziwa bado unahitajika kuongezeka zaidi kwasababu ulaji wa maziwa upo.

“Mpaka sasa ng’ombe milioni 2 nchini huzalisha maziwa hivyo tunampango wa kuongeza ng’ombe wa maziwa zaidi bado tunaamini wigo bado upo”. Amesema Prof.Elisante 

Amesema ili uzalishaji na uchakataji uongezeke lazima soko la ndani na nje liweze kuwa kubwa.

Aidha, Prof.Elisante amesema unywaji wa maziwa nchini kwa siku ni zaidi ya lita milioni 8.3.

“Kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo duniani FAO kila mtu wa kawaida anatakiwa anywe lita 200 kwa mwaka lakini sasa Tanzania mwaka 2019 tulikuwa tumefikia lita 49 lakini mwaka 2020 tumefikia lita 54 kwa mwaka”. Amesema Prof.Elisante 

Pamoja na hayo amewataka wenye Viwanda kuongeza ubora wa uzalishaji wa maziwa ili kuweza kumnufaisha mnyaji wa maziwa nchini.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, amewataka wananchi kupendelea kunywa maziwa kwasababu yana protini, wanga na virutubisho vingi vinavyosaidia kuimarisha afya.

Nae Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa Khamis amesema wataendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kama vilabu vya Jogging na wengine wengi kuzalisha bidhaa zilizobora hapa nchini.

Hata hivyo kwa upande wake Mwenyekiti wa Dar Jogging Bw.Ramadhan amesema kutokana na unywaji wa maziwa kuwa chini wameamua kufanya mbio hizo ili kuhamasisha unywaji ea maziwa.

Amesema muitikio umekuwa mkubwa kwa maana zaidi ya vilabu 94 vimeshiriki katika mbio hizo zilizotumia saa moja mpaka walivyomaliza.

 

No comments :

Post a Comment