Kauli hiyo imebainishwa na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Mhe. Selemani Jafo wakati akitoa taarfa ya uchaguzi wa wanafunzi wa
kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2021 leo jijini Dodoma.
Akizungumza Mhe. Jafo amesema
kuwa kati ya wanafunzi 4,169 wamechaguliwa kujiunga na shule za bweni
ambapo wanafunzi 970 watajiunga na shule za wanafunzi wenye ufaulu mzuri
Zaidi.
Pia Mhe. Jafo amesema kuwa
wanafunzi 1,238 watajiunga na shule za ufundi, wanafunzi 1,961
watajiunga na shule za bweni za kawaida.
Wanafunzi 755,537 wakiwemo
wavulana 362,247 na wasichana 385,665 wamechaguliwa kujiunga na shule za
Sekondari za kutwa katika maeneo mbali mbali nchini.
“Miongoni mwa waliochaguliwa,
wanafunzi wenye mahitaji maalum ni 2,491 wakiwemo wavulana 1,312 na
wasichana 1,179 sawa na asilimia 75.0 ya wanafunzi wenye ulemavu
waliofanya mtihani huo.
Mhe. Jafo ameeleza kuwa jumla ya
mikoa tisa ya Kagera, Katavi, Lindi, Mtwara, Mwanza, Njombe, Ruvuma,
Songwe na Tabora imeweza kupangia shule wanafunzi wote waliofaulu
kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021.
Hata hivyo jumla ya wanafunzi
74,166 sawa na asilimia 8.9 wakiwemo wavulana 34,861 na wasichana 39,305
hawakupangiwa shule katika awamu ya kwanza kutokana na uhaba wa vyumba
vya madarasa.
“Hivyo wanafunzi wenye sifa ambao
hawakupangiwa shule katika awamu hii ya kwanza watapangiwa shule katika
awamu ya pili kabla ya tarehe 28 Februari, 2021”, ameeleza Mhe. Jafo
Kwa kuongezea Mhe. Jafo amesema
kuwa wanafunzi hao wataendelea kupangiwa shule kadri Mikoa na
Halmashauri zitakavyoendelea kukamilisha vyumba vya madarasa na madawati
hadi kufikia tarehe 28 Februari, 2021.
Aidha amewaagiza walimu na
watendaji wa sekta ya Elimu katika ngazi zote kuongeza bidii katika
usimamizi na ufuatiliaji wa utoaji wa elimu ili kufikia malengo ya elimu
yaliyopangwa na serikali.
“Ninatoa wito kwa viongozi wa
Mikoa na Halmashauri kushirikiana na wadau wa elimu kukamilisha majengo
na kuandaa mazingira ya kuwapokea wanafunzi wote waliochaguliwa kuanza
masomo yao mwezi Januari, 2021 bila vikwazo vya aina yoyote”, ametoa
wito Mhe. Jafo.
Vile vile amesema kuwa wakuu wa mikoa na halmashuri kuhakikisha wanafunzi wote wanaripoti shuleni kwa wakati.
Mhe. Jafo amesema kuwa mzazi au
mlezi ambaye atakuwa na hoja yoyote juu ya uchaguzi wa wanafunzi afike
Ofisi za Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri husika ili aweze
kuhudumiwa ipasavyo.
Aidha anaweza kupiga simu katika
kiyuo cha huduma kwa wateja katika Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa namba ya
simu 026-2160210 AU atume ujumbe mfupi wa (SMS) au WhatsApp kwa namba ya
0735160210
No comments :
Post a Comment