Tuesday, December 15, 2020

WAZIRI AWESO AWATAKA DAWASA KUHAKIKISHA WANAONGEZA MIKOA YA KIHUDUMA WANANCHI WAPATE MAJI

Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelezo ya mradi wa Mkuranga Phase I kwa Waziri wa Maji Jumaa Awesu wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi huo unaotarajiwa kumaliza mwezi Februari 2021.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelezo ya chanzo cha maji cha mradi wa maji Mkuranga Phase I kwa Waziri wa Maji Jumaa Awesu. Waziri Awesu amefanya ziara ya kutembelea mradi wa maji Mkuranga Phase 1 unaotarajiwa kumaliza mwezi Februari 2021.

Waziri wa Maji Jumaa Awesu akikagua ujenzi wa kituo cha kusukumia maji ( booster pump) kitakachokuwa na uwezo wa kusukuma maji Lita Milion 6 katika mradi wa maji Mkuranga. Awesu amefanya ziara ya kutembelea mradi wa maji Mkuranga unaotarajiwa kumalizika Februari 2021

……………………………………………..

Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuongeza mikoa ya kihuduma ili kuwafikia hadi wananchi wa

pembezoni mwa mji.

Hayo ameyasema wakati wa ziara ya kutembelea mradi wa maji wa Mkuranga, naa kuitaka Dawasa kuongeza mikoa kutoka 15 na iwe mingi zaidi.

Akizungumza baada ya kutembelea mradi huo, Awesu ameupongeza uongozi wa Dawasa chini ya Afisa Mtendaji Mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha wana mkuranga wanapata maji safi na salama.

“Dawasa mnafanya kazi kubwa sana, kwa sasa mna mikoa 15 ya kihuduma, mnatakiwa kuongeza mikoa ya kihuduma ili muwafikie hadi wananchi wa pembezoni msitoe huduma maeneo ya mjini tu,” amesema Aweso.

Aweso amesema Dawasa wanafanya kazi kubwa sana, watambue maji hayana mbadala na baada ya kuwakabidhi mji wa Mkuranga wameanza kuona uelekeo na wahakikishe wana Mkuranga wanapata maji safi na salama.

“Mradi huu mnasema hadi mwezi wa pili utakuwa umekamilika Phase 1, Dawasa kama mnaweza kuongeza nguvu hata ikiwezekana mwezi wa kwanza nije kuuzindua wana Mkuranga waanze kupata maji,” Aweso

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga ameishukuru Dawasa kwa jitihada kubwa wanazozifanya za kuhakikisha tatizo la maji ndani ya Mji wa Mkuranga linafikia tamati.

Mradi wa maji Mkuranga – Vikindu unatarajia kumaliza mwanzoni mwa mwaka 2021 ukiwa na thamani ya Bilion 5.5 za kitanzania utakaohudumia wakazi 25,500.

Ujenzi huo unahusisha ujenzi wa tanki kubwa la maji lenye ujazo wa Lita milioni 1.5, kituo cha kusukumia maji. (Booster pump station) chenye uwezo wa kusukuma maji lita 6 kwa saa na kulaza mtandao wa bomba za kusambaza maji wa Km 63.5 kwa Phase 1.

Mradi huo unatumia chanzo cha maji kutoka kisima namba HB EB 4B chenye kina cha 545m na uwezo wa kutoa maji lita 284,400 kilichopo eneo la Mkwali tumbo Mkuranga Mjini

 

No comments :

Post a Comment