**************************
Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.
Tume ya Sayansi
na Teknolojia COSTECH imewakutanisha wanahabari na watafiti mbalimbali
hapa nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo namna ya tafiti hizo kuwafikia
walaji kwa njia rahisi kwa kutumia wanahabari.
Akizungumza
wakati wa kufungua mafunzo hayo yaliyofanyika Jijini Dodoma Mkurugenzi
wa Menejimenti ya maarifa kutoka COSTECH Dkt Philibert Luhunga amesema
lengo ni kuona teknolojia ya Sayansi inayobuniwa na watafiti inawafikia
wananchi au walaji kwa lugha rahisi.
“Lengo la
kuwakutanisha hapa ni tafiti mbalimbali zinazofanywa na hawa watafiti
ziwafikie wananchi kiurahisi kwa sababu tafiti hizo zinakuwa katika
Lugha ya Sayansi, lakini tafiti hizo zikipelekwa kwa wananchi kwa
kutumia wanahabari ni rahisi kueleweka na walaji wa tafiti hizo” amesema
Dkt Luhunga.
Amewataka
waandishi wa habari kuandika mara kwa mara habari zinazohusu Sayansi
hasa tafiti zinazofanywa na wataalamu wetu ili wananchi wanufanike na
tafiti zinazofanywa na wataalamu wetu.
Amesema hasa
katika kipindi hiki nchi imejipambanua kuwa nchi ya viwanda Teknolojia
za ndani ni muhimu sana maendeleo ya Taifa ili kama nchi tufikie azima
ya kuwa nchi ya Viwanda.
Amebainisha kuwa
tayari wameshafanya semina kama hizo katika Mikoa ya Dar es saalam,
Tanga, Mtwara na Unguja na katika maeneo hayo kumeonekana matokeo chanya
kwa waandishi kuwa na mwamko mkubwa wa kuripoti na kuandika habari za
utafiti mbalimbali.
“Kote ambako
tumefanya semina kama hizi kumeonyesha mwamko mkubwa Sana wa kuripoti
taarifa za Sayansi na kitafiti zilizosaidia kuokoa maisha ya watu, hasa
tafiti za hali ya hewa kwa kanda ya mashariki” amesema.
Aidha amewashauri
wananchi kuendelea kufuatilia habari za utafiti wa kisayansi katika
nyanja mbalimbali na wasisite kuwasiliana na Mamlaka husika wanapoona
mabadiliko ya kisayansi katika maeneo yao.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa kituo cha TARI Makutupora Dkt Cornel Masawe amesema
waandishi wa habari ni watu muhimu katika kufanikisha usambaaji wa
tafiti za Kisayansi kuwafikia walengwa wa tafiti hizo.
Amesema kwa
upande TARI wanavituo kumi na saba (17) nchini nzima ambavyo vinafanya
utafiti wa mbegu mbalimbali za mazao na wamekuwa wakizalisha Teknolojia
tofauti tofauti za mbegu za kilimo zinazoweza kuwanufaisha wakulima hapa
nchini.
Amebainisha kuwa
hapo mwanzo walikuwa wakitumia siku ya 88 kutangaza tafiti zao tukio
lililokuwa likifanyika mara moja kwa mwaka lakini Sasa wamefungua Ofisi
katika kanda zote hapa nchini katika ofisi za maonyesho ya 88 na vituo
hivyo vitakuwa wazi wa siku zote ili kuwahudumia wakulima.
No comments :
Post a Comment