wafanyakazi
wa shirika la umeme Tanesco wakiwa katika picha ya Pamoja Mara baada ya
waziri mkuu kufungua kongamano la 11 la wanunuzi na ugavi lililofanyika
katika ukumbi wa AICC
Mkuu wa ununuzi na ugavi kutoka shirika la umeme Tanesco Nyalu Mwamaja akiongea na waandishi wa habari.
baadhi ya washiriki wakipata maelekezo katika Banda la Tanesco lilopo katika kongamano hilo
……………………………………………………………………………………….
Na Woinde Shizza , ARUSHA
Wito
umetolewa kwa wataalam wa ununuzi na ugavi kufuata sheria kanuni na
taratibu zilizowekwa ili kuweza kukuza uchumi wa nchi yetu.
Hayo
yamebainishwa na mkuu wa idara ya ununuzi kutoka shirika la umeme
Tanesco Nyalu Patson Mwamwaja wakati akiongea na waandishi wa habari
Mara baada ya kupokea hati ya shukrani ya kuthamini mkutano wa 11
ununuzi na ugavi uliofanyika katika ukumbi wa AICC uliopo mkoani Arusha
Alisema
kuwa vyema wakaacha uzembe na wafanye kazi kwa weledi katika
kusimamia mnyororo wa ununuzi na ugavi iliwasikwamishe utekelezaji wa
miradi.
Alisema
kuwa wameamua kuthamini kongamano hilo kwakuwa wao ni wadau wakubwa na
shirika hilo kunatoa mchango mkubwa Sana katika fani hii ya ununuzi na
ugavi
Alisema
shirika la Tanesco ndilo linaloongoza kwa kuajiri wanunuzi wengi na
wagavi ,ambao ni wafanisi na wanaoleta Maendeleo katika ufanisi endelevu
wa nchi na wa fani hii kwa ujumla ,na waendelee kufanya kazi vyema kwa
ajili ya Maendeleo ya nchi yetu.
Aliwataka
waendelee kufuata sheria kanuni za maadili na kuendelea kutoa ushauri
wa manunuzi kwa kufuata Sheria ya manunuzi ya umma .
No comments :
Post a Comment