Kushoto jaji mstaafu Dkt Fauz Twaib akizindua moja ya chapisho kwa ajili ya kusaidia wanasheria msaada wa kisheria kulia ni Rais wa Chama Cha mawakiliTanganyika (TLS)Dkt Nshala Rugemela
Jaji mstaafu Dkt Fauz Twaib akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kufungua mkutano huo
…………………………………………………………………………………………
Na Woinde Shizza ,ARUSHA
CHAMA
Cha mawakili Tanganyika (TLS) kimewakutanisha wanataaluma wa anuai
(professional diversity )800 kujadili maswala mbalimbali wanayokumbana
nayo ,kujua fursa ,changamoto zilizopo katika taaluma zao haswa kwa
upande wa Sheria .
Akiongea
katika mkutano wa kwanza wa anuai za kitaaluma ulioandaliwa na
Chama hicho uliofanyika mkoani Arusha Jana Rais wa Chama hicho
Dkt.Nshala Rugemeleza alisema kuwa wamekutana kujua fursa zilizopo
katika kila taaluma ,kuangalia ni jinsi gani wanasheria wanaweza
kushirikiana na watu wa taaluma mbalimbali nakuweza kufanya shughuli zao
kwa ufanisi mkubwa zaidi pamoja na kupanua wigo wa shughuli zao ili
kuweza kwa pamoja kuwedadisi fursa zilizopo.
Alisema
kuwa sheria huwezi kufanya peke yako Kama sheria ilivyo ni vyema
ukajua watu wa kada mbalimbali wanafanya kitu gani , maana sheria za
nchi yetu zinagusa kada zote na fani zote lakini mwisho wa siku
nijukumu la mwanasheria kutoa tafsiri ya hizo sheria
“Bunge
limeweza kutunga sheria ambazo zinagusa karibu fani zote lakini
mwisho wa siku mwanasheria ndio anatakiwa atowe mwongozo wa hizo sheria
kwa kila kada,Ila watu wa kada hizi wamekuwa wakitaka kutoa tafsiri zao
ni vyema watu wakaweza kukutana na kujadili namna gani wanaweza
kashirikiana na wanasheria ,wasanifu wa majengo ,wanahabari ,wahasibu
ili kujenga ushirikiano na kuweza kukuza fursa na kutumia teknolojia za
kisasa kuweza kukuza uwanda wa ufanyaji wa kazi” alibainisha Rugemeleza
Akifungua
mkutano huo jaji mstaafu Dkt .Fauz Twaib alisema kuwa mkutano huo
utawawezesha wadau hao kushirikiana kwa pamoja na kuboresha njia bora
zaidi za kutoa huduma.
“Kwa
Sasa kumekuwa na wimbi kubwa la mawakili ,wametoka kwenye idadi
mawakili Chini ya elfu moja miaka 10 iliopita na kufikia elfu 10 sasa
katika hali ya aina iyo na upya wa mawakili wengi unasababisha
changamoto kuwa nyingi Sana ,kwa ujumla kuna matukio mengi zaidi
yanaoyoonekana kuonyeshwa Kuna aja ya kuangalia namna gani mawakili
wanafanya kazi pamoja na maswala ya ueledi wao wa kufanya
kazi”alibainisha Twaib
Akiongelea
machapisho mbalimbali aliyoyazindua leo kwa ajili ya wanasheria alisema
kuwa yatawasaidia kujua sheria mbalimbali ambazo hawazijui kwani hakuna
mwanasheria ambaye anajua sheria zote papo kwa papo hivyo machapisho
hayo yatamsaidia kujua kwa haraka kwani yamefupishwa.
Kwa
upande wake wakili mstaafu Dkt Hawa Sinare alisema kuwa machapisho haya
ni miongozo mzuri kwa wanasheria haswa wageni kwani itakuwa inawasaidia
hata hawa wanasheria wachanga kujua Sheria ambazo walikuwa hawayajui.
No comments :
Post a Comment