Thursday, December 3, 2020

Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wahimizwa kujiunga na Akademi ya Huawei ili kuongeza ujuzi kwenye fani ya TEHAMA.

Afisa wa Huawei, George Harrison akizungumzwa wakati wa semina hiyo.


 Mkuu wa Chuo cha COICT, Dk Mussa Kissaka akizungumzwa kwenye semina hiyo.

 Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ndaki ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (COICT) wametakiwa kuchukua fursa ya kujiunga na Shule ya mafunzo ya Huawei katika Chuo hicho

katika Programu ya ujuzi wa TEHAMA. Wito huo ulitolewa na Mkuu wa Chuo cha COICT, Dk Mussa Kissaka katika semina ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Akiongea kwenye semina hiyo Dk Mussa Kissaka alisema, Shule ya mafunzo ya TEHAMA ya Huawei inatoa jukwaa la kujifunza ambapo wanafunzi watapata nafasi ya kujifunza Teknolojia za kisasa za Huawei ambazo zitawasaidia kuziba pengo la maarifa ya TEHAMA na ujuzi wa teknolojia hiyo.

Huawei husaidia Vyuo Vikuu kukuza vipaji katika nyanja ya TEHAMA ambayo inakidhi mahitaji ya tasnia, ikitoa vipaji vya hali ya juu kwa maendeleo ya tasnia na taifa kwa ujumla.

 “Tunajisikia furaha kwa ushirikiano huu kwani wanafunzi wetu wanapewa mafunzo yanayohusiana na TEHAMA na baadaye hupewa vyeti ili waajiriwe kwa urahisi. Wanapata uelewa wa vifaa na teknolojia za Huawei ambavyo vinatumika pia katika tasnia ya mawasiliano. Wanachopata kutoka kwa akademi ya Huawei ni nyongeza ya kile wanachofundishwa katika chuo chetu, hivyo inawaongezea fursa Zaidi kwenye soko la ajira.” Alisema.

Aidha Dk. Kissaka alitoa wito kwa wanafunzi wapya kuwahi fursa ya kujiunga na akademi ya Huawei ili  kujiongezea ujuzi katika tasnia ya mawasiliano inayokua haraka.

"Hata kampuni kubwa za simu nchini zinatumia vifaa imara vya Huawei na utaalam katika uendeshaji wa huduma zao, kwa hivyo, inawaweka mahali pazuri katika kupata nafasi za kuajiriwa," akaongeza.

Huawei imeunda mfumo wa vipaji na ujuzi katika tasnia ya TEHAMA unaozingatia mchakato mzima wa mafunzo, udhibitisho, na ajira - kwa kuimarisha utaratibu wa ushirikiano kati ya Vyuo Vikuu na biashara, ikilenga kukuza maendeleo ya tasnia na kubuni mifano ya kukuza vipaji kulingana na mahitaji ya biashara.

 Afisa wa Huawei, George Harrison alielezea kuwa kampuni ya Huawei inawaleta wanafunzi wa TEHAMA katika Ulimwengu halisi wa soko la ajira kwa kutafsiri kivitendo kile wanachojifunza darasani.

Huawei imekuwa ikiandaa Mashindano ya TEHAMA kila mwaka, na kushirikisha maelfu ya wanafunzi kutoka vyuo tofauti tofauti barani Afrika na dunia nzima. Ushindani huo unawaweka wanafunzi wa TEHAMA katika ramani ya ajira kwani wengine wanaajiriwa kikamilifu, wengine wanapata tarajali na wengine kudhaminiwa nafasi za kujiendeleza kimasomo.

"Tumekuwa tukiwafundisha wanafunzi ustadi wa TEHAMA katika Ulimwengu wa teknolojia kwa kuwapa nafasi za kuwa wataalam katika sekta ya TEHAMA," alisema Harrison.

Bwana Harrison pia ameongeza kuwa Huawei kwa kushirikiana na Wakala wa ‘E-Government’ (EGA-ambayo inasimamia utumiaji wa TEHAMA katika kutoa huduma za serikali) itaandaa mkutano wa ana kwa ana kwa wanafunzi wote wa TEHAMA ili kuwatambulisha sokoni.

Mnamo 2013, Huawei ilizindua akademi yake ya TEHAMA, mradi wa ushirikiano wa biashara ya elimu ambao unajumuisha taasisi za elimu ya juu, kusaidia kujenga mfumo wa ikolojia wa vipaji katika tasnia hiyo. Kwa miaka sita iliyopita, Huawei imewekeza sana katika kuchunguza mafunzo kwa Vyuo Vikuu na kutumia uzoefu huo.

No comments :

Post a Comment