Wednesday, December 16, 2020

Wakulima wa Parachichi Njombe Wapewa Vyeti Vya Ubora na Kituo Cha Kimataifa Cha Biashara ITC

Wakulima wa zao la Parachichi ambalo limebatizwa jina la Dhahabu ya kijani kutokana na kuongezeka kwa mahitaji yake sokoni,wamesema kitendo cha kituo cha kimataifa cha biashara ITC kuwapa vyeti vya ubora vinavyotambuliwa kimataifa kitawafanya kudhibiti biashara chafu iliyokuwa ikifanywa na baadhi ya wafanyabiashara kutoka nchini Kenya ambao walikuwa wanachukua malighafi hiyo hapa na kisha kuigonga nembo ya nchi yao jambo lilikuwa linaua soko la Tanzania.

Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa vyeti vya ubora wawakilishi wa wakulima 600 kutoka kwenye vikundi 8 vya mkoa wa Njombe na kikundi 1 kutoka mkoa wa Mbeya akiwemo Steven Mlimbila,Transit Nyika na Lucy Kilasi wanasema kwa kipindi kirefu wamekuwa wakihujumiwa na wafanyabishara wa kenya hivyo kitendo cha kituo cha biashara cha kimataifa kuwatambua kinafungua milango kwao kwenda moja kwa moja sokoni badala ya kupitishia Kenya.

Awali akitoa msimamo wa serikali katika sekta ya kilimo hususani Parachichi mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya amesema wataendelea kuweka mazingira rafiki kwa wakulima na wawekezaji  pamoja na kutafuta masoko ya uhakika kwa malighafi zinazozalishwa nchini.

Lakini nini faida ya kutambuliwa kimaifa Sokonni huyu hapa ,Safari Fungu ni mratibu wa mradi wa Markup unaotekelezwa na kituo cha kimataifa cha biashara ITC unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya EU anasema itasaidia wakulima kufatiliwa kwa urahisi pamoja na kuwaunganisha na masoko

 

No comments :

Post a Comment