Wednesday, December 16, 2020

TAFITI ZA KILIMO ZATOA MATOKEO CHANYA – BASHE


Mhe. Hussein Bashe Naibu Waziri wa Kilimo, akiwa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bahi akipokea taarifa ya utekelezaji wa Maagizo yake aliyoyatoa Mwezi June 2020
Mhandisi wa Umwagiliaji Mkoa wa Dodoma,Raphael  Laiza akipokea Maagizo ya Mh. Waziri Bashe, hayupo katika picha, kwenye ukumbi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Bahi.
Kulia, Mkulima wa Bahi Sokoni Sechelela Mbigili akizungumza  kuhusu athari za mafuriko katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya Bahi sokoni, kushoto
ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali

Mhe.Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akiangalia sampuli ya ngano iliyofanyiwa majaribio kwenye skimu ya kilimo cha Umwagiaji Bahi Sokoni.

NaibuWaziriwaKilimo Hussein Bashe akikagua sehemu ya Madaraja yaliyojengwa na Kampuni ya SGR ili kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
…………………………………

NA MWANDISHI WETU, BAHI

Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema tafiti  za kilimo cha

ngano katika mikoa ya Dodoma, Mbeya na Arusha zilizofanyika hivi karibuni zimetoa matokeo chanya ambapo aina tatu za mbegu za ngano zilizofanyiwa
majaribio zimeonyesha uwezo mkubwa wa kustawi  nakutoa mavuno ya kuridhisha katika mikoa hiyo.

Akizungumza wakati wa ziara ya kikazi wilayani Bahi , Naibu Waziri Bashe amezitaka taasisi za  Utafiti wa kilimo (TARI), Taasisi ya Mbegu (ASA), Tume ya Taifa ya Umwagiliaji(NIRC)  pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao nchini (DCD) kushirikiana katika kutekeleza mpango  wakilimo hicho ili kupata
matokeo chanya.

“Hatua hiyo inakwenda sambamba na sera ya Maendeleo ya  Taifa ya mwaka 20 – 25 inayoelekeza taifa kuzalisha zao la
ngano  kwawingi ili kusitisha uagizaji wa bidhaa hiyo nje ya nchini.” Alisisistiza

Naibu Waziri Bashe alimaliza  kwa kusema kuwa, kwa kuanzia zoezi hilo litatekelezwa katika Skimu kumi na nne  Wilayani Bahi.

 

No comments :

Post a Comment