Thursday, December 17, 2020

TPSC YAPONGEZWA KWA KUTUMIA FEDHA ZA MAPATO YA NDANI KUJENGA JENGO LITAKALOBORESHA UTOAJI MAFUNZO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika akizungumza na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) – Kampasi ya Tabora (hawapo pichani) alipoenda kukagua jengo jipya la TPSC Kampasi ya Tabora.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzani-Kampasi ya Tabora alipoenda kukagua jengo jipya la TPSC Kampasi ya Tabora.

Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika akiwasilisha kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika taarifa ya mradi wa jengo jipya la TPSC-Kampasi ya Tabora alipoenda kukagua jingo hilo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika akishuhudia mpangilio wa vitabu katika maktaba maalum iliyoko kwenye jengo jipya la Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) – Kampasi ya Tabora.

 Baadhi ya wanafunzi wakipata mafunzo katika moja ya darasa lililopo ndani ya jengo jipya la Chuo Cha Utumishi wa Tanzania (TPSC) -Kampasi ya Tabora lililojengwa kwa fedha za mapato ya ndani. Mwonekano wa jengo jipya la Chuo Cha Utumishi wa Tanzania (TPSC) – Kampasi ya Tabora lililojengwa kwa fedha za mapato ya ndani.

***********************************

Na. James K. Mwanamyoto – Tabora

Tarehe 17 Disemba, 2020

Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kimepongezwa kwa kutumia fedha za mapato

yake ya ndani kiasi cha shilingi bilioni 3.5 kujenga jengo la ghorofa mbili lililoanza kutumika kutoa mafunzo kwa Watumishi wa Umma na Wananchi katika fani mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho kwenye Kampasi ya Tabora.

Pongezi hizo zimetolewa leo Mkoani Tabora na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika mara baada ya kukagua jengo jipya la TPSC Kampasi ya Tabora.

Mhe. Mkuchika amesema hatua ya kutumia fedha za ndani kujenga jengo lenye ofisi na madarasa, linapaswa kuigwa na taasisi nyingine za umma ambazo zinaitegemea Serikali kuwapatia fedha kuboresha ofisi zao.

“Kitendo cha kutumia fedha za ndani kwa maendeleo ya taifa ni jambo zuri ambalo Mhe. Rais amekuwa akisisitiza mara kwa mara, hivyo, ujenzi wa jengo hili linanipa ujasiri wa kuwaalika Viongozi wa Kitaifa kulizindua rasmi, huku kipaumbele kikiwa kwa Mhe. Rais mwenyewe,” Mhe. Mkuchika amefafanua.

Mhe. Mkuchika ameongeza kuwa, ushirikiano na uadilifu uliopo baina ya Viongozi na Watumishi ndio ulifanikisha kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo, hivyo amewataka kuuendelea na utamaduni huo kwa masilahi ya chuo na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa jengo hilo, Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika amesema jengo hilo limekamilika na kuanza kutumika kabla ya uzinduzi rasmi ili kuongeza ufanisi kiutendaji na kubaini mapungufu yanayoweza kujitokeza kwa lengo la kuyadhibiti.

Mradi wa ujenzi wa jengo hilo linalojumuisha maktaba, vyumba vya madarasa ya kompyuta, kumbi, madarasa ya kawaida na ofisi za watumishi ulianza tarehe 5 Novemba, 2014 na kukamilika rasmi tarehe 26 Machi, 2020.

fafanua kuwa, TAKUKURU inatakiwa kuwajengea wananchi imani ya kiutendaji ili pale inapotokea wananyang’anywa haki zao na mtu au taasisi yoyote kwa njia za rushwa, TAKUKURU ndio iwe ni kimbilio lao huku wakiwa na imani kuwa watasaidiwa ipasavyo na taasisi hiyo.

“Nawasihi endeleeni kuwang’ata wala rushwa na mafisadi wote ili mradi msimuonee au kumpendelea yeyote, na endeleeni kuifanya haki ndio nguzo ya utendaji kazi wenu wa kila siku”, Mhe. Mkuchika alihimiza.

Awali, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi Sabina Seja akitoa maelezo kuhusu jengo hilo alisema, uzinduzi wa jengo la TAKUKURU wilaya ya Namtumbo ni ushaidi tosha kuwa Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imeonesha nia na dhamira ya dhati ya kukabiliana na vitendo vya rushwa, ubadhilifu wa mali za umma nchini.

Bibi Seja, amemtibitishia Mhe. Mkuchika kuwa, watumishi wa TAKUKURU wilayani Namtumbo watatumia jengo la ofisi hiyo kuhakikisha wanapambana na vitendo vya rushwa, ufisadi na ubadhilifu kwa manufaa ya wananchi na maslahi ya taifa.

Mhe. Mkuchika amefungua jengo hilo la TAKUKURU wilaya ya NAMTUMBO, ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambaye tangu aingie madarakani amefanya kazi kubwa ya kuimarisha na kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi nchini.

 

No comments :

Post a Comment