Thursday, December 17, 2020

SHABAN BRUNO, MBUNIFU WA NYUMBA ALIYEAJIRI VIJANA 17







Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam.

ANAFAHAMIKA zaidi kama Mr Gypsum, Shaban Bruno (32) mzaliwa wa jijini Mbeya ambaye amekuwa maarufu zaidi katika mitandao ya kijamii hasa

Facebook na Instagram kutokana na ubunifu wa kipekee na urembo wa nyumba (interior designer.)

Akizungumza na Michuzi Blog, Shaban amesema amekuwa mtaalamu wa kazi hiyo aliyoianza rasmi mwaka 2011 na baadaye kuanzisha kampuni yake inayofahamika kwa jina la 'Gypsum Gang.'

Amesema katika kuhakikisha anafanya kazi bora aliwainua vijana wengine wapatao kumi na saba na wanafanya kazi katika Mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani.

Aidha amesema kuwa kujiajiri kumemsaidia katika kuinua kipato chake binafsi pamoja na vijana anaoshirikiana nao katika kufanya nao hizo.

Shaban amewashauri vijana kutumia fursa zinazojitokeza na kujiajiri wenyewe pamoja na kuwashika mkono vijana wengine pindi wanapofanikiwa

No comments :

Post a Comment