Mkurungenzi wa Miliki TBA Bw.Said Mndeme ,akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua ukarabati wa nyumba za Serikali zilizo chini ya TBA katika eneo la Area D jijini Dodoma.
Msimamizi wa Mradi wa Ukarabati wa nyumba za Area D,Dismas Liwenga,akitoa maelezo kwa waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu jinsi walivyojipanga na timu yake kukamilisha ukarabati huo ndani ya wiki nane.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkurungenzi wa Miliki TBA Bw.Said Mndeme baada ya kukagua ukarabati wa nyumba za Serikali zilizo chini ya TBA katika eneo la Area D jijini Dodoma.
Mkazi wa Eneo la Area D Yustadi Athanas,akitoa shukrani kwa TBA kwa kuamua kukarabati nyumba za eneo hilo na kuziweka katika mazingira bora ya kuishi.
Baadhi ya mafundi wakiendelea na ukarabati wa nyumba za Eneo la Area D zilizo jijini Dodoma.
Mkurungenzi wa Miliki TBA Bw.Said Mndeme (katikati) akiendelea na ukaguzi wa ukarabati wa nyumba za Serikali zilizo chini ya TBA katika eneo la Area D jijini Dodoma.
……………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Wakala Majengo nchini (TBA) imewataka wapangaji wote wanaoishi katika nyumba za serikali
zilizo chini ya wakala hao kulipa kodi zao za pango kwa haraka ili kurahisisha ukarabati wa nyumba hizo unaoendelea maeneo mbalimbali nchini.Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurungenzi wa Miliki TBA Bw.Said Mndeme baada ya kukagua ukarabati wa nyumba hizo unaoendelea katika eneo la Area D jijini Dodoma.
”Napenda toa rai kwa wapangaji wote nchi kulipa kodi zao kwa haraka ili tuendane na kasi ya ukarabati wa nyumba hizi haya yote yanaendana na Pesa ambazo zinatokana na kodi”amesema Mndeme
Aidha amesema kuwa wameanza ukarabati wa nyumba na majengo ya viongozi katika mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma ambapo Dar es salaam wana ukarabati wa nyumba 84 na katika eneo hili la Area D kuna majengo 45 pia ukarabati unaendelea vizuri.
Hata hivyo amesema kuwa ukarabati unaoendelea katika eneo hili la Area D tumeanza na ukarabati wa Pa na kuboresha sehemu ambazo huwa zinafunja pamoja na kupaka rangi na kuweka alama za TBA.
Mndeme amesema kuwa Serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni tano kwa ajiili ya ukarabati wa nyumba hizo nchi nzima ambapo hapo awali nyumba hizo kwa zaidi ya miaka 30 hazikukarabatiwa.
Aidha amesema kuwa ukarabati huo wa nyumba pamoja na majengo ya viongozi unatarajia kukamilika Februari mwakani na nyumba zote zitakuwa katika mazingira bora.
Kwa upande wake Msimamizi wa Mradi wa Ukarabati wa nyumba za Area D,Dismas Liwenga amesema kuwa katika mapango kazi wake amejipanga kukamilisha ukarabati huo kwa kipindi cha wiki nane.
Aidha ameongeza kuwa ukarabati unaoendelea kwa sasa ni ukarabati wa nje pamoja na mifumo ya maji taka.
Baadhi ya wakazi wa nyumba hizo wameishukuru serikali kwa ukarabati huo ambao umeleta unafuu wa kuishi katika nyumba zenye hadhi.
Ukarabati wa nyumba hizo za Serikali zilizo chini ya TBA unaoendelea kwa sasa unafatia agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli mwaka 2017 alipoelekeza baadhi ya nyumba takriban 2311 ambazo zilikuwa chini ya Halmaahauri mbalimbali kurudishwa Serikali kuu.
No comments :
Post a Comment