*Vijana washauriwa wasipoteze fursa ya Tamasha
KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na
Pwani imeandaa tamasha kubwa la 'Twenzetu kwa Yesu' litalofanyika Desemba 19 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.Akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dkt. Emmanuel Luvanda amesema Tamasha hilo litafungua fursa mbalimbali kwa vijana katika kujitambua na kwenda na malengo ya kiuchumi.
Amesema Tamasha hilo linafanyika kwa mara ya tatu na limekuwa na mchango mkubwa kwa vijana kwa imani zote.
Dkt. Luvanda amesema vijana wajitokeze kwa wingi kwenda kujifunza licha ya kupata na burdani za neno la Mungu.
Aidha amesema Tamasha limekuwa na baraka na kimbilio kwa vijana kukutana na kumtukuza kwa uimbaji na mafundisho yanayowajenga kiroho, na kimwili kutoka watumishi wa Mungu.
Kauli mbiu ya Tamasha ni, ''Kijana umechaguliwa'' ikiwa na maana kijana utapata kile ambacho ulikuwa unahitaji na sasa unakwenda kukipata.
Mgeni Rasmi katika Tamasha hilo ni Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dkt.Alex Malasusa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Upendo Media Nengida Johanes amesema katika katika Tamasha hilo litakuwa na waimbaji wa nje na ndani huku waimbaji wa ndani ni Joel Lwaga, Joshua Mlelwa, Hype Squad, Rungu la Yesu, Neema Gospel Choir, Jerusalem Choir Kimara, TAFES Ardhi huku wa mwimbaji wa nje akiwa ni Mikhululi Bhebhe wa Afrika Kusini.
Amesema watakaotoa semina ni wachungaji mashuhuri ambao Lewis Hiza wa KKKT na Samwel Kabigi wa Kanisa la Morovian.
No comments :
Post a Comment