Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa ujenzi Luteni Kanali George William Nyisa wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya ofisi mpya za Ikulu Chamwino, Dodoma, leo Desemba 8, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua sehemu mbali mbali wakati akikagua ujenzi wamajengo ya ofisi za Ikulu Chamwino, Dodoma, leo Desemba 8, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua sehemu mbali mbali wakati akikagua ujenzi wamajengo ya ofisi za Ikulu Chamwino, Dodoma, leo Desemba 8, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia mafundi wa kiraia wakati akikagua ujenzi wa majengo yaofisi za Ikulu Chamwino, Dodoma, leo Desemba 8, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wajenzi wa kijeshi baada ya kukagua majengo ya ofisi za Ikulu Chamwino, Dodoma, leo Desemba 8, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wajenzi wa kijeshi baada ya kukagua majengo ya ofisi za
Ikulu Chamwino, Dodoma, leo Desemba 8, 2020 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiongea na mmoja wa askari wajenzi walati akikagua majengo ya ofisi za Ikulu Chamwino, Dodoma, leo Desemba 8, 2020
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 08 Desemba, 2020 amekagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Ikulu
Mkoani Dodoma na kuelezea kuridhishwa na kiwango na kasi ya ujenzi wa
majengo ya ofisi hizo unaofanywa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Ujenzi
wa Ofisi hizo ulioanza tarehe 17 Februari, 2020 unatarajiwa kukamilika
katika kipindi cha miezi 3 ijayo na unafanywa kwa usanifu na muonekano
sawa na Ofisi za Ikulu zilizopo Jijini Dar es Salaam.
Msimamizi
wa ujenzi wa ofisi hizo, Luteni Kanali George William Nyisa amemueleza
Mhe. Rais Magufuli kuwa ujenzi huo utakamilika kwa wakati uliopangwa.
Akikagua
majengo yanayojengwa, Mhe. Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa kwake
na uimara wa nguzo na kuta zinazojengwa na amesema ni fahari kubwa kwa
Taifa kujenga ofisi yake ya Ikulu kwa kutumia Jeshi badala ya kutumia
wakandarasi kutoka nje ya nchi.
Mhe.
Rais Magufuli pia amezungumza na Vijana wa JKT wanaoshiriki ujenzi huo
ambapo amekumbusha ahadi yake kuwa vijana hao 2,424 wataandikishwa
katika JWTZ mara watakapomaliza jukumu la ujenzi wa Ofisi za Ikulu.
Pamoja
na kuwapongeza vijana hao, Mhe. Rais Magufuli pia amewapongeza vijana
wa kiraia wanaoshiriki katika ujenzi huo ambao ni mafundi, na amewaahidi
kuwa atawaangalia mara baada ya kumaliza kazi hiyo.
No comments :
Post a Comment