Sunday, December 13, 2020

Mkandarasi atakiwa kumaliza Jengo la Ofisi za Halmashauri kabla ya 2021.


Mshauri Elekezi kutoka TBA Mhandisi Haruna Kalunga akitoa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo na wataalamu wengine alioambatana nao.  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akisikiliza maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya halmashauri ya Wilaya ya Laela kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo John Msemakweli (wa pili toka kushoto) nyuma yao ni matofali yatakayotumika katika ujenzi wa ofisi hiyo. 

*************************************

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amemuagiza Mkandarasi Suma JKT

anayejenga Ofisi za halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kumaliza jengo hilo kabla ya mwaka mpya wa 2021 baada ya jengo hilo kudumu kwa miaka zaidi ya mitatu bila ya kukamilika.

Mh. Wangabo amesema kuwa Pamoja na kufahamu changamoto kadhaa za ujenzi zilizoikumba eneo hilo hali iliyofanya ujenzi wa msingi wa jengo hilo kuchukua muda mrefu kutokana na eneo hilo kujaa maji na hivyo mkandarasi kuomba kuongezewa muda wa kumalizia jengo hilo lakini ameongeza kuwa hatua hiyo imeshapita.

“Mkandarasi aliomba ‘extension’ kadhaa nay a mwisho inaisha tarehe 31 Disemba yam waka huu, sasa nikuangize mkandarasi uzingatie huo mkataba, mkataba huo wa tarehe hiyo niliyoisema ufuatwe, kazi zifanyike usiku na mchana, leo ni tarehe 11 bado kama wiki tatu, hili jingo linapaswa kukamilika vinginevyo tutatafakari hatua ya kuchukua kwasababu tumeshakaa muda mrefu miaka mitatu haikubaliki,” Alisema.

Aidha, alitahadharisha kuwa fedha inayotolewa kwaajili ya ujenzi wa jingo hilo kutumika kwaajili ya malengo ya ujenzi wa jingo hilo na sio badala yake Mkandarasi huyo kubadili matumizi ya fedha hizo kutokana na taratibu zao za kuweka fedha za miradi yao sehemu moja na hatimae kubadili matumizi.

Hata hivyo wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi huo mshauri elekezi Kaimu Meneja Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Mkoa wa Rukwa Mhandisi Haruna Kalunga amesema kuwa miongoni mwa changamoto wanazopata ni Pamoja na mshitiri kuchelewa kufanya malipo kwa wakati hali inayosababisha ucheleshwaji wa ujenzi huo.

“Kwa mfano hati ya madai namba 5 ilipitishwa na Mshauri Elekezi tarehe 5.6.2020 ila ilikuja kulipwa tarehe 5.10.2020 takriban miezi minne mkandarasi alikuwa anasubiria malipo, changamoto ya pili ni kuchelewa kupatikana kwa mkandarasi mdogo wa huduma, mpaka unaona jingo hili linaanza kutumika hadi leo halina miundombinu ya umeme,” Alieleza.

Ujenzi huo wenye thamani ya Shilingi 3,494,444,696/= unaojumuisha ujenzi wa vymba vya ofisi 137, jingo la mgahawa, uzio wa mita 427, kibanda cha mlinzi na maegesho ya magari ulianza tarehe 27.10.2017 na kutarajiwa kumalizika tarehe 25.5.2019 lakini hadi leo tarehe 11.12.2020 umefikia 56% huku mkandarasi akiwa amelipwa hati 5 za madai zenye jumla ya shilingi 1,869,535,687.55/= ambazo ni saw ana 45% ambapo gharama hizo ni bila ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

Katika Hatua nyingine Mh. Wangabo amepongeza juhudi zinazofanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa kutumia fedha zake za mapato kuendelea na ujenzi wa ofisi za halmshauri hizo wakati wakisubiri fedha kutoka serikalini lakini pia kuanzisha ujenzi wa Stendi ya Mabasi katika mji mdogo wa Laela ambao ndio makao makuu mapya ya Halmashauri hiyo baada ya agizo la Rais Mh. John Pombe Magufuli kuzitaka halmashauri hizo kuhamia katika maeneo yao ya kiutawala.


 

No comments :

Post a Comment