Baadhi ya washiriki wa kongamano la kupinga
ukatili wa kijinsia wakicheza muziki wa taarabu uliokuwa ukipigwa na wanamuziki
wa bendi ya DSMA Women.
Wanamuziki wa bendi ya DSMA Women wakitoa
burudani wakati wa kongamano hilo.
Naibu Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier wakimpongeza Diana Mbogo kutoka Millennium Engineers baada ya kutoa maelezo ya jinsi wanavyofanya shughuli zao wakati wa kongamano hilo.
Mmoja wa maofisa wa Ubalozi wa Ufaransa
akiangalia ubunifu wa wajasiriamali wa kazi za mikono wakati wa kongamano hilo
Naibu Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson (wa tatu kushoto) akiwa makini kuangalia filamu iliyokuwa inazungumzia ukatili wa kijinsia wakati wa kongamano hilo.
Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kwenye kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia lililoandaliwa na Ubalozi wa Ufaransa nchini.
Baadhi ya wasanii wakitoa burudani ya nyimbo wakati wa kongamano hilo la kuzungumzia ukatili wa kijinsia likiendeleaSehemu ya washiriki waliohudhuria kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia wakiangalia filamu fupi iliyokuwa inazungumzia masuala ya ukatili wa kijinsia wakati wa kongamano hilo.
Naibu Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia lililoandaliwa na Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania.
Wasanii wakiendele kuonesha ubunifu wao wa sanaa katika kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa kutokomeza ukatili wa kijinsia.Naibu Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson (katikati) akijadiliana jambo na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier (kushoto).
Naibu Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson (katikati) akijadiliana jambo na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier (kushoto).
Naibu Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson (katikati) akiwa na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier (kushoto) na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya (kulia) wakifuatilia burudani kutoka kwa kundi la wasanii waliokuwa wakitumia sanaa yao kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia.Waliosimama ni sehemu ya walioshiriki kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia lililoandaliwa na Ubalozi wa Ufaransa nchini.
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
KONGAMANO la kupinga ukatili wa kijinsia ambalo limeandaliwa na
Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania limefana kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza wakiwemo wanafunzi wa vyuo vikuu huku Naibu Spika Dk.Tulia Ackson akitumia nafasi hiyo kuiomba jamii kuendelea kushiriki kikamilifu kukomesha matukio ya ukatili wa kijinsia kwani bado yameendelea kutokea.Amesema siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zimeisha Desemba 10,2020 lakini ni vema katika siku 365 za mwaka zikawa ni za kupinga ukatili huo wa kijinsia hasa kwa kuzingatia kauli mbiu iliyokuwa inatumiwa katika siku hizo 16 ilikuwa inasema "Mabadiliko yanaanza na mimi".
Dk.Tulia Ackson amesema hayo jana usiku kwenye kongamano hilo lililokuwa limeandaliwa na Ubalozi huo wa Ufaransa nchini Tanzania kwa kushirikiana na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya.
Kongamano hilo lilitawaliwa zaidi na burudani kupitia wasanii mbalimbali waliotumia sanaa kuzungumzia matukio ya ukatili wa kijinsia sambamba na hotuba mbalimbali za viongozi ikiwemo iliyotolewa na Dk.Tulia na Balozi wa Ufaransa nchini ....
Akizungumza wakati wa kongamano hilo , Dk.Tulia amesema kwamba "Hizi siku 16 za kupinga na kutokomeza ukatili wa kijinsia kimsingi kilichofanya ni kuamsha mjadala ili kila mtu ashiriki kwasababu ujumbe unasema Mabadiliko yananza na mimi , kila mtu afahamu kila siku ,ni siku ya kupinga na kutokomeza ukatili wa kijinsia.
"Hivyo zile siku 16 zilikuwa za kumsha mjadala zimefungwa siku ya leo(jana Desemba 10,2020) lakini tunatamani siku 365 za mwaka kila mmoja aseme inaanza na mimi na kusitokee ukatili wa kijinsia mahali kokote.
"Kwa hiyo siku ya leo nimekuja kushiriki tukio hili ambalo limeandaliwa vizuri na na Ubalozi wa Ufaransa kwa kushirikana na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya, lakini pia na nchi ya Ujerumani na Nedhaland, kwa hiyo ninawapongeza sana, ni tukio zuri limewaleta vijana wa kike na kiume pamoja kwa hiyo wamepata fursa ya kujadili kwa pamoja.
"Na ni vizuri kuwaweka watoto wa kike na wa kiume pamoja kwani wataweza kusonga mbele kwa hatua kwasababu wote watakuwa na mawazo na kuwa na muelekeo mmoja wa kuangalia namna ambavyo hutakiwi kufanya ukatili wa kijinsia kwa yoyote.
Kuhusu nafasi ya nchi katika kukomeha ukatili wa kijinsia , Dk.Tulia amesema kama nchi imepiga hatua lakini bado kunahitajia hatua zaidi kwani bado matukio ya ukatili wa kijinsi ni mengi na yameendelea kutokea na hata katika wiki hizi mbili amesikia mkoani Pwani Pwani kuna mume kamchinja mkewe,
"Tumesikia Manyara kuna watoto watatu mama yao amewaua, lakini nimesikia tena kuna mwanaume amepigwa na mwanamke, kwa hiyo matukio bado yapo lakini kitakwimu tunapunguza.Tunataka ukatili wa kijinsia utokomee kabisa, kwa hiyo bado tunatakiwa kuchukua hatua zaidi.
Wakati wa kongamano hilo , baadhi ya washiriki wameeleza kufurahishwa na uamuzi wa Ubalozi wa Ufaransa kuandaa kongamano hilo kwani imekuwa fursa kwao kujadiliana kwa kina kuhusu mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.
No comments :
Post a Comment