Tuesday, December 29, 2020

MBUNGE WA MAKETE ASOTA BARABARANI AKISAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO YA BARABARA IPELELE






KUTOKANA na Mvua nyingi zinazoendelea kunyesha wilayani Makete, mawasiliano ya barabara ya Makete-kwenda Mbeya kupitia Ipelele

yamekatika kwa muda sasa kitu kilichopeleka Mbunge wa Makete Ndg Festo Sanga kufika eneo la tukio kusaidiana na wananchi kuitatua kero hiyo.

Sanga aliyewasili mlima wa ipelele majira ya saa mbili asubuhi hii leo amefika na kusaidia kutatua changamoto hiyo kwa kusaidiana na wananchi kukwamua gari ya wasafiri iliyokuwa inakwenda mbeya. 

Pamoja na jitihada hizo, Mbunge aliwasiliana na  TANROAD mkoa wa Njombea ambao kwa uharaka wamefika eneo la tukio leoleo na kesho mkandarasi atakuwa eneo la kazi kuanzia asubuhi ili kuhakikisha changamoto hiyo inatibika ili wasafirishaji na wasafari waweze kufanya shughuli zao kwa ufanisi.

Mbunge huyo amesisitiza,nia ya serikali ya kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami ipo na tayari mkakati wa serikali kuanza ujenzi upo njiani unakuja, hivyo anawekeza nguvu zake kwa serikali kuikumbusha umuhimu wa barabara hiyo na zingine zinazoiunganisha makete mf. chimala-Matamba-Kitulo na ile ya Kipengele Lupila.

Makete inachangamoto kubwa ya barabara kutokana na mvua nyingi zinazo nyesha kwa muda mrefu na wakati huo huo magari makubwa ni mengi yanayoingia kupakia dhahabu ya makete(Mbao,Viazi na matunda,) hivyo uhitaji wa barabara ya lami ni mkubwa sanaa.

 

No comments :

Post a Comment